Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Cresentius Magori akifafanua jambo kwa washiriki wa kongamano la Maofisa Rasilimali watu wa Taasisi za Kifedha lililofanyika Morogoro Hotel.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Maoafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi za Kifedha wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa kongamano hilo.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Rasilimali watu NSSF ,Chiku Matessa akizungumza na maafisa Rasilmali watu wa mabenki na taasisi mbali mbali za kifedha wakati wa uzinduzi wa kongamano la maafisa rasilimali watu wa mabenki.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF, Chiku Matessa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Moafisa Rasilimali Watu (HR Forum) lililofanyika Morogoro Hotel.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekutana na maafisa rasilimali watu wa mabenki 35 yaliyopo Nchini katika ukumbi wa Morogoro Hotel.
Kongamano hilo linalojulikana kama HR FORUM hufanyika kila mwaka kwa kuwashirikisha Maafisa Rasilimali watu kutoka taasisi za kifedha.
Lengo la Kongamano hili likiwa ni kutoa elimu juu ya Shughuli za NSSF, Mafao yanayopatikana na huduma nyinginezo kama Hiari Scheme, Wakulima Scheme, WESTADI na Bima ya Matibabu.
Pia kwenye kongamano hilo watoa mada walizungumzia juu ya mabadiliko ya kikokotozi cha Pensheni ambacho kimetangazwa na kupitishwa na mdhibiti wa Mifuko (SSRA), kwa mifuko yote.
Akizungumza kwenye Kongamano hilo Meneja Mafao wa NSSF, James Oigo alisema "Kikokotozi hicho kinamfanya mwanachama wa NSSF kuwa mwanachama atakayepata pensheni kubwa kuliko mwanachama wa mfuko mwengine wowote".