Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

FERGUSON ABWAGA MANYANGA KUINOA MAN UNITED

$
0
0
Kocha wa Man United, Sir Alex Ferguson


LONDON, England

Mskochi huyo aliyetwaa mataji zaidi ya 30 katika miaka yake 26 ya kuinoa Manchester United, vikiwamo vikombe 13 vya Ligi Kuu ya hapa, anatarajia kuaga mashabiki katika mechi ya mwisho ya ligi msimu huu, ugenini dhidi ya West Bromwich Albion, Mei 19.

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anatarajia kustaafu, kuhitimisha zaidi ya robo karne ya kufanya kazi Old Trafford, klabu hiyo imetangaza rasmi leo Jumatano.

Fergie, 71 ameiongoza klabu kwa mafanikio ndani na nje ya uwanja, akiingiza klabu hiyo katika soko la hisa la New York Stock Exchange, huku ikikusanya maaamilioni ya mashabiki duniani kote kuanzia mwaka 1986 aliposhika hatamu.

Katika miaka yake 26 ya kuinoa Man United, Fergusonraia wa Scotland ametwaa zaidi ya mataji 30, yakiwamo 13 ya Ligi Kuu ya England– pamoja na huu iliotwaa msimu huu.

Fergusonanatarajia kuaga mashabiki wa klabu hiyo baada ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu msimu huu, ugenini dhidi ya West Bromwich Albion, itakayopigwa Mei 19, taarifa ya klabu ya Manchester United ilisema.

CNN



Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>