Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akipeana mkono na aliyekuwa Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Mchungaji
Peter Msigwa ambaye amejiondoa kutoka chama hicho na kujiunga rasmi na Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Juni 30, 2024, jijini Dar Es Salaam.
Msigwa
amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza uhalali
wa kuwa mkosoaji wa CCM, lakini pia kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti
wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa
anayofanya ya kuiongoza nchi na kuwatumikia Watanzania. Pia baada ya
kuchoshwa na siasa za uongo, unafiki na kiulaghai zinazofanywa na
Chadema.
↧
Rais Dkt. Samia ampokea rasmi Msigwa wa CHADEMA
↧