
Polisi walifika nyumbani kwa Mansoor asubuhi na kupekuwa na kugundua vitu hivyo baada ya kupata taarifa toka kwa wasamaria wema kuonesha wasiwasi wao juu ya Mansoor.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Naibu Msaidizi Mkuu wa Upelelezi Zanzibar Salum Msangi aliwaambia waandishi wa habari kwamba pamoja na umiliki wa silaha hizo upo kisheria lakini anapaswa kuwa na risasi za short gun 50 ambapo risasi za bastola kisheria anatakiwa awe nazo 25 kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Risasi 5 zimetumika polisi wanafuatilia zimetumika vipi. Mansour anakuwa ni kiongozi wa kwanza katika historia ya Zanzibar kukutwa na kiasi kikubwa cha Risasi zikiwa zimefichwa nyumbani kwake.