BAADA ya wasanii wa kundi la Mapacha, kutambulisha ngoma yao mpya inayojulikana kwa jina la ‘Time for the Money’ waliodai kumshirikisha nyota wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu, msanii huyo amekana ushiriki huo.
Wimbo huo umetambulishwa Juni 23 na kusambazwa katika vituo mbalimbali vya redio na umetengenezwa na katika studio za Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Sorround Saund chini ya mtayarishaji mahiri nchini, Tudy Thomas.
Kwa mujibu wa Lulu kupitia ukarasa wake wa instagram, aliandika kuwa hana taarifa ya kushirikishwa na mapacha anashangaa kuona jina lake linatumika na kupewa hongera na baadhi ya watu.
“Mbona mnaninyanyasa jamani hamuishi kunipa matukio, nina uhakika sina wazo lolote na huku kushirikishwa, labda kama kuna Lulu mwingine ambaye anatumi jina langu waliomshirikisha, mlio sikia huu wimbo naombeni mnisaidie maana nashirikishwa kimiujiza jamani,” aliandika nyota huyo.
Lulu aliendelea kuwaonya wasanii ambao wanatumia jina lake kwaajili ya manufaa yao binafsi kuachana na hiyo tabia.