Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 0

$
0
0
MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL  AMKARIBISHA MAKAMU WA RAIS WA CHINA NA UJUMBE WAKE IKULU DAR LEO, WASAINI MIKATABA
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisainiana mkataba na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, wa Makabidhiano ya gari la matangazo la Shirika la Utangazaji la TBC, yaliyofanyika mapema mwaka huu. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao. Picha na OMR
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, (kulia) akisainiana mikataba miwili na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, ya makubaliano ya ushirikiano wa Kitaalamu utakaoiwezesha China kuwapa mafunzo Wanariadha wa Tanzania nchini China na wa makubaliano ya awamu ya tatu ya Ushirikiano wa kiufundi baada ya China kusaidia na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Taifa. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>