Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani za Uchaguzi ya TFF, Julius Lugaziya (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi wa kamati hiyo kumrudisha mgombea wa Rais katika klabu ya Simba, Michael Wambura. Kulia Mkurugenzi Msaidizi Sheria na Wanachama TFF, Eliud Mvella.(Picha na Francis Dande)
Baadhi ya mashabiki wanaomuunga mkono mgombea wa nafasi ya Rais wa klabu ya Simba, Michael Wambura wakishangilia nje ya ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kamati ya Rufaa ya TFF, kumrejesha katika kinyang’anyiro hicho.