Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 3

$
0
0
WAKULIMA WA CHAI BUMBULI KUMFIKISHA MAKAMBA MAHAKAMANI
UMOJA wa Wakulima wa Chai (UTEGA), katika Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga, unatarajia kumburuza mahakamani Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.

Hatua hiyo inakuja baada ya Utega kubaini kuwa kiwanda hicho kilifungwa kwa kuchochewa na Mbunge wa Jimbo hilo  kwenye mkutano wake wa hadhara wa Mei  26, 2013 uliofanyika ndani ya kiwanja kilichopo kiwandani hapo.


Uamuzi  huo wa UTEGA wa kumshitaki mbunge huyo ambaye  pia  ni  Naibu Waziri wa Sayansi na Teknelojia, umefikiwa katika Mkutano Mkuu maalum wa UTEGA uliyofanyika hivi karibuni wilayani Lushoto.

Wajumbe wa mkutano huo waliiagiza Mponde Tea Estates Company Ltd, iende mahakamani kupata kibali cha kufungua kiwanda ili wakulima wasiendelee kuteseka. 

Kwa mujibu wa mkutano huo, mashitaka mengine ambayo wanakusudia kufungua mahakamani ni kudai fidia iliyotokana na kufungwa kiwanda hicho na kukisababishia hasara kubwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa UTEGA, William Shelukindo alisema kuwa kwa takribani mwaka mmoja tangu kiwanda kifungwe jitihada mbalimbali zimechukuliwa za kukinusuru zikiwemo kufanya kikao na Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ya mkoa wa Tanga.

Shelukindo alisema kuwa katika mkutano huo, Kamati ya siasa ya mkoa iliagiza  kufanyika kwa uchaguzi Mkuu  wa Usambara Tea Growers Association (UTEGA), kama ilivyopendekezwa na Mbunge Makamba.

Hata hivyo,  Shelukindo alisema kuwa kikao cha Kamati ya utendaji ya UTEGA cha Septemba 14, 2013,  hakikuafikiana na maagizo hayo.

“Kamati yetu ya utendaji ilipingana na wazo la Kamati ya siasa ya CCM Mkoa kwa sababu kubwa kwamba, endapo tutafanya  uchaguzi kabla ya wakati, tutakuwa tumekiuka Katiba ya UTEGA,”  Shelukindo alisema.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa walifanya kikao kingine kati ya uongozi wa UTEGA, na maafisa wa Hazina (Msajili wa Hazina), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na Msimamizi wa mali za serikali zilizouzwa (CHC) Consolidated Holiding Copretion.

Akifafanua zaidi Shelukindo alisema kuwa kikao kilibainisha wazi kwamba suala la Kiwanda cha Chai cha Mponde ni la kisheria kwa vile kiwanda pamoja na Shamba la Sakare viliuzwa na serikali kwa UTEGA, na hakuna upande wowote wenye tatizo na umoja huo.

Hata hivyo,  mwenyekiti aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, Mwenyekiti wa Lushoto Tea Company  Nawab Mulla alifanya kikao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda, Februari 23, mwaka huu, mkoani Dodoma.

Alisema kuwa katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu alishauri kwamba kiwanda kifunguliwe kwani wakulima wa chai wanateseka sana na suala hilo linamuumiza kichwa chake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>