Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original Victoria kimaro katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014 chini ya udhamini wa Kinywaji cha Redd’s Original kulia ni Hashim Lundenga toka kamati ya Miss Tanzania na kushoto ni Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original, pamoja na Kamati ya Miss Tanzania leo wamezindua rasmi kuanza kwa mchakato wa kumpata “Redds Miss Tanzania 2014/2015.
Akizungumzia Udhamini wa mashindano ya mwaka huu Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Bi. Victoria Kimaro alisema “Redds Original, ina furaha kubwa siku ya leo kutangaza udhamini wa mashindano ya kumsaka mrembo atakayemrithi Happines Watimanywa (Redds Miss Tanzania wa sasa).
Nina imani wote tunakumbuka kuwa mwaka 2012 Redds ilisaini mkataba na Lino International wa kudhamini mashindano haya maarufu na yenye hadhi yake hapa nchini kama mdhamini mkuu kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2014, hivyo huu ukiwa ni mwaka wetu wa tatu kwa mujibu wa mkataba, tunayo furaha kubwa kusema kuwa Redds Original imeweza kutoa mchango wake kwa jamii ya kitanzania, hususan tasnia hii ya Urembo.” Alisema Victoria

Akizungumzia udhamini wa kinywaji cha Redds Original, mkurugenzi mkuu wa Lino International, Hashim Lundenga alisema; Lino International ina kila sababu ya kuipongeza Redds Original, kwani zaidi ya kuwa mdhamini mkuu kwa miaka mitatu kinywaji cha Redds kimekuwa mdau mkubwa wa mashindano haya kwa miaka mingi.
Kwa niaba ya Lino International na wadau wa tasnia ya Urembo tunawapongeza sana Redds Original kwa imani yao kubwa na mashindano haya ambayo hakika sasa yanavutia zaidi.
Kwa niaba ya Lino International na wadau wa tasnia ya Urembo tunawapongeza sana Redds Original kwa imani yao kubwa na mashindano haya ambayo hakika sasa yanavutia zaidi.
Tuna imani kubwa kuwa mwisho wa mkataba huu wa miaka mitatu sio mwisho wa mahusiano mazuri kati ya Lino International, wadau wa Urembo na kinywaji cha Redds Original.
Aidha nawataka waandaaji wote wa mashindano haya kuanzia ngazi za vitongoji hadi kanda kufanya maandalizi mazuri na pia kufanya taratibu kwa kuzingatia masharti yaliyopo katika mkataba na mdhamini wetu mkuu kinywaji cha Redd’s pasipo kwenda kinyume.