Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 0

$
0
0
Rebecca Malope kutumbuiza Tamasha la Pasaka
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi April 20. (Picha na Francis Dande)
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.

 Na Francis Dande

  MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, msanii huyo amepata kura nyingi kutoka kwa mashabiki waliompendekeza.

“Tunashukuru kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki tuliwasiliana na Rebecca ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na kutukubalia ombi letu. Lakini pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu nyingine huko kwao, hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo tamasha litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na ratiba yake,” alisema Msama na kuongeza.

“Lakini niwahakikishie mashabiki wetu kwamba, msanii huyo tutakuwa naye na sasa ni suala la Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo na kisha nasi tumweke kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi.”

Rebecca amewahi kutamba na albamu za ‘Saturday Nite’ aliyoitoa Januari 1, 2009, ‘Hlala Nami’ Novemba 11, 2003, ‘Siyabonga’ Desemba 21, 2000, ‘Free at Last’ Novemba 18, 1997, ‘African Classics’ Mei 5, 2009 na ‘Greatest Hits’ Januari 10, 2006.

Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro na Rose Muhando wote wa Tanzania na Sarah K wa Kenya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>