Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Young Killer ameipongeza serikali kwa kuamua kurudia kutoa upya matokea ya kidato cha nne ya mwaka jana.
Akizungumza jijini Dae es Salaam, Young Killer alisema wanafunzi wengi waliohitimu mwaka jana walikua hawana imani na matokeo hayo, hivyo haya yeye atafarijika akiona matokeo yamerudiwa upya.
“Kiukweli wengi tunajua kwa matokeo hayo tumeonewa, mimi nitaona kweli nimefeli halali endapo matokeo ya pili yataonesha hivyo lakini kwasaivi naamini kama walinipa matokeo ya mntu mwingine,” alisema msanii huyo ambaye ni miongozi mwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka jana.