Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 5

$
0
0
UGONJWA WA SARATANI YA MATITI WATISHIA MAISHA YA AKINAMAMA WENGI-TANZANIA
Mkurugenzi Mkuu wa Asasi ya Saratani ya Matiti nchini, Angela Kuzilwa (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano  na waandishi wa habari jijini Dar ers Salaam, leo. Kushoto ni Kezia Makoyo na Mweka Hazina wa taasisi hiyo, Gloria Akida. (Picha na Francis Dande)

Na Mwandishi Wetu

Asasi ya Saratani ya Matiti imesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kasi kubwa ya ongezeko la maradhi ya saratani ya matiti.

Akizungumza na wandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Asasi hiyo, Angela Kuzilwa, alisema kuna hatari baada ya miaka 20 wanawake wote nchini wakaja wakajikuta wanakabiliwa na maradhi hayo.

Alisema  hali hiyo inatokana na uelewa mdogo walionao wanawake kuhusu maradhi hayo ambayo yanaonekana kuongezeka kwa kasi kubwa kila kukicha.

Angela alisema kutokana na mazingira hayo Asasi hiyo imepanga kutembelea baadhi ya mikoa hivi karibuni ikiwemo Tanga, Morogo na Iringa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu maradhi hayo.

“Watu wanaokufa kwa saratani ni wengi kuliko wanaokufa kutokana  na maradhi ya TB, Malaria na Ukimwi,”alisema Angela.

Angela aliwataka wanawake hao kujitokeza mara kwa mara hospitalini kwa ajili ya kupima afya zao, endapo watabainika kuwa na maradhi hayomapema waweze kupatiwa tiba.

Alisema ugonjwa huo unatibika endapo utaanza kutibiwa katika hatua za awali na sio wangoje hadi umekuwa sugu ambako katika hali kama hiyo itakuwa ni vigumu kutibiwa.

Aliongeza kuwa maradhi hayo ya saratani ya titi, tafiti zinaonesha kwamba hukuna sababu maalumu inayojukana kusababisha maradhi hayo.

Angela alivitaja vichocheo vinavyoweza kusababisha saratani hiyo kuwa ni matumizi ya kemikali, uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi, utumiaji wa vyakula vya mafuta kupita kiasi.

Vingine kuanza tendo la ndoa mapema, kutofanya mazoezi kwa wale watu wanene, kuopata mtoto kabisa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>