Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 3

$
0
0
Soko la Kariakoo @ Coco Beach lazinduliwa
Meneja Masoko wa Hazina Capital, Rachel Ndauka (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi wa soko jipya la Kariakoo @ Coco Beach, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko Msaidizi,Cartas Maganga. (Na Mpiga Picha Wetu)


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Hazina  Capital ya jijini Dar es Salaam, imezindua soko jipya la biashara litakalojumuisha wafanyabiashara wa bidhaa za aina mbalimbali kutoka Kariakoo na kuwapa nafasi ya pamoja ya kuonesha na kuuza bidhaa zao katika Fukwe za Coco, zilizoko Oysterbay.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rachel Ndauka ambaye ni Meneja Masoko wa Hazina Capital, alisema soko hilo jipya litajulikana kwa jina la Kariakoo @ Coco Beach, ambalo litaanza kazi rasmi kuanzia Machi 29 na 30 na kuendelea kila mwisho wa wiki.

Ndauka aliongeza kuwa, Kariakoo @ Coco Beach, litatoa nafasi kwa wananchi wasioenda ama wanaoenda Kariakoo, kununua bidhaa walizokuwa wakizipata huko kwa bei ile ile, lakini safari hii wakizipatia katika Fukwe za Coco, zikiwa na punguzo maalum.

Aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika Fukwe za Coco wakiwa na familia zao, kila mwisho wa wiki, kwa ajili ya kujipatia huduma zilizo bora na mahitaji muhimu ya kifamilia waliyokuwa wamezoea kwenda kuyapatia Kariakoo.
Alibainisha kuwa lengo la Kariakoo @ Coco Beach , sio tu kuwafanya watu wanunue bidhaa hizo, bali kuwasogezea huduma muhimu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na foleni na usalama wa wateja waendapo mjini.

Ndauka alisisitiza kuwa, Kariakoo @ Coco Beach ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kukuza pato lao na kutanua biashara zao, huku pia wakitumia ujio wa soko hilo kulitangaza Soko Kuu la Kariakoo, lililoko katikati ya jijini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>