Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Mahakama zisigeuzwe Misukule ya kuwatisha Watanzania

$
0
0
Bryceson Mathias
PAMOJA na Tume ya Wajumbe wa Rasimu ya Katiba kusahau kuutaja Donda Ndugu na ugonjwa Mkubwa wa nchi hii, wananchi walio wengi wametaka Mhimili wa Mahakama usigeuzwe Msule wa kuwatishia watanzania.kwa kutumiwa na wanasiasa.
Kati ya Watu 10 waliohojiwa kuhusu Rasimu hiyo ya hivi karibuni, Wanne wamezilalamikia Mahakama, Wanne Rushwa na Ufisadi uliokithiri, na Wawili wamelialamikia Polisi, kama vyombo vinavyoweza kuharibu Mchakato mzuri wa Katiba
Kada mkongwe wa Chama Tawala (CCM) aliyetaka asitajwe asiandamwe alisema, Rasimu ya Katiba itakuwa nzuri tu, kama Viongozi wa Mahakama watakataa wasitekwa na kutumiwa na wanasiasa Kama Misule ya kutishia watanzania.
Amedai, Wakuu wa Wilaya, na Vyombo hivyo viwili Mahakama na Polisi, kwa siku za karibuni, mbali ya kulalamikiwa na wananchi, lakini katika tafiti kadhaa vimetuhumiwa kuwa vinara wa Rushwa na kuubeba Ufisadi kwa mbereko ya kisiasa.
Mwananchi Lukas Sungi Kitindi wa Dar yeye alisema, Wajumbe wa Rasimu hiyo  wameacha Shaka kwa kutoainisha katika Kabrasha zima (Document), Katiba itasemaje kuhusu Janga na Ndonda Ndugu lililooza la Rushwa na Ufisadi uliokithiri.
Wanawake wawili kati ya Watano waliohojiwa ukiwaondoa wanaume watano walisema, Rasimu imeacha Utata kwa kutoweka wazi juu ya utendaji wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) amabayo wanadai iwajibike kwa wananchi si kwa Rais
Mchungaji aliyeomba asitajwe kwa sababu zake binafsi alisema, Watanzania wanatakiwa kuwa na Musa ambaye akiwa Mlimani, alipoinua Mikono wana wa Israel walishinda Vita,  ambapo iliposhuka Wa-Ameleki walishinda.
Alisema wasaidizi wawili waliokwenda naye, walilazimika kuchukuwa Jiwe Musa akae, ndipo washikilie Mikono isishuke bila wao kuinua Mikono, kwa sababu wangeinua Mikono na Musa wangechoka, na ushindi wa Israel usingepatikana.
Ni Rai yangu kwamba, ili tuondokane na baadhi ya Wabunge na wanasiasa Maslahi, Watanzania tunatakiwa kumtazama Musa ambaye hahitaji Rushwa, Ufisadi, na Maagizo ya wanasiasa Uchwara, ili kutoa hukumu ya Ushindi dhidi ya Wa-ameleki.
Wajibu wetu kama Musa, ni kutekeleza maagizo ya Mungu kuinua Mikono Juu Israel waendelee kushinda, ili baadhi yetu wanapodanganyika na Ubwabwa, Kofia, Tisheti na Skafu, basi wainuke watanzania waliokwenda na Musa Mlimani waweke jiwe akalie na tushikilie Mikono.
Tukiwaachia Rasimu hiyo baadhi ya wanasiasa Maslahi ambao bungeni ni ndiyoooo, na James Mbatia akidai Iundwe Tume dhidi ya Elimu wanakataa! Ajabu haohao leo wamegeuka iundwe Tume waliyoipinga! .
Wananchi; Msiwasikilize wala kuwakubali hawatufai, maana wanaoshusha mikono ya Musa mlimani ili Wa-ameleki waendelee kutupiga hadi tushindwe kuendesha kukidhi Ugumu wa maisha, huku wao wakifaidi.
Rushwa na Ufisadi unaofanywa na kufumbiwa macho na watawala, ni sawa na Vitisho vya Goliati kwa wana Israel. Ndivyo vinavyowafanya Walimu wasiipende kazi yao kwa kunyimwa haki zao. Hivyo kwa Rasimu hii, watanzania tuna Kazi Moja tu!
Kati ya Mawe matano aliyookota Daudi, alihitaji Jiwe Moja tu litakalotua kwenye Kipaji cha Goliati ili kubadilisha Kilio cha Wana wa Israel na kupeleka Shangwe Yerusalemu kwenye nchi ya Maziwa na Asali! Jiwe hilo ni kura yako 2015.
Jiwe hilo la Kombeo, Likitua kwenye kipaji cha Goliati, Rushwa, Ufisaji, Dhuluma ya  Haki, Vitisho na Mauaji ya watu wasio na hatia vinavyofanywa na wenye Mamlaka! Vitakwisha, na Israel itakuwa Huru!

Benki ya Exim yatunukiwa tuzo ya utunzaji bora wa mazingira mwaka 2013

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant (kulia) wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani katika viwanja vya Zakhem Mbagala Jumatano. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (Kushoto) akimkabidhi kombe Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant (kulia) baada ya benki yake kutunikiwa tuzo ya utunzaji bora wa mazingira katika kipengele cha taasisi za fedha katika Tuzo za Mazingira Manispaa ya Ilala mwaka 2013. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili ushoto) akimkabidhi kombe Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant (kulia) baada ya benki yake kutunikiwa tuzo ya utunzaji bora wa mazingira katika kipengele cha taasisi za fedha katika Tuzo za Mazingira Manispaa ya Ilala mwaka 2013. Akishuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Exim mara baada ya kuikabidhi benki hiyo kombe baada ya kuibuka washindi katika kipengele cha taasisi za fedha katika Tuzo za Mazingira Manispaa ya Ilala mwaka 2013. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant (kulia) akionyesha cheti walichoshinda benki yake katika kutambua mchango wa benki hiyo kwenye utunzanji wa mazingira wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2013 jijini Dar es Salaam Jumatano. Katika ni Kaimu Meneja Masoko Anita Goshashy. 

Na Mwandishi Wetu


BENKI ya Exim imeibuka mshindi wa jumla kwa taasisi za fedha kwenye Tuzo za Mazingira zilizoandaliwa na Manispaa ya Ilala kwa Mwaka 2013.

 Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango ya taasisi mbali mbali nchini katika utunzaji wa mazingira. Sherehe za utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika viwanja wa Zakhem, Mbagala na kuandaliwa na Wilaya ya Temeke ikiwa sehemu ya kuhadhimisha Siku ya Mazingira Duniani iliyoambatana ka kauli mbinu ya “Fikiri, Kula, Tunza”.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki ambaye alikuwa mgeni rasmi aliitahadharisha jamii kutunza mazingira wanayoishi ili kuwa na miradi endelevu.

“Mahali popote ambapo mazingira yameharibiwa hata uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara utapungua siku hadi siku,” alisema. Alisema kuwa mkoa wa Dar es Salaam unachangamoto changamoto mbali
mbali katika masuala ya utunzaji mazingira zikiwemo usimamizi hafifu wa  sheria ndogo ndogo za hifadhi ya mazingira. “Kuna watu wanakiuka na wengine wanagomea lakini mkumbuke mnavofanya
hivyo mnajijengea maisha duni.

 Sheria hizi zinazowekwa naomba sana mzisimamie kwa manufaa ya taifa letu.

“Hatuna budi kutii sheria hizi bila shuluti na tukifanya hivyo Dar es Salaam yetu itakuwa sehemu nzuri sana pa kuishi,” aliongeza. Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant mara baada
ya kupokea tuzo hiyo alibainisha mikakati na jitihada za benki yake za kuendelea kuunga mkono kampeni mbali mbali za utunzaji mazingira nchi nzima.

Grant alisema kuwa kuna umuhimu kwa wadau wote kushirikiana kwa pamoja ili kuongeza nguvu katika utunzaji wa mazingira hali ambayo itasaidia kuongeza mapinduzi ya uchumi wa kijani (green economy) ili kuboresha maisha ya jamii na kupunguza mazingira hatarishi kwa ujumla.

“Benki ya Exim itaendelea  kuunga mkono jitihada za mapinduzi ya
uchumi wa kijani. Tunahitaji kuiacha sayari ikiwa na mazingira
endelevu kwa vizazi vijavyo.

“Mabadiliko makubwa yanatakiwa kufanwa haraka kama tunakitaji kupiga
hatua kweli. Lazima matendo yetu na maamuzi ya kimazingira tunayofanya
yalete mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika maisha ya kila mmoja
wetu nchini,” aliongeza Grant.

UVUNJAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

$
0
0

 Mwendesha Bajaj akivunja sheria za usalama barabarani kwa kupita katika pembeni mwa barabara na kuweza kusababisha ajali kama alivyokutwa katika mtaa wa Shaurimoyo.

BENKI YA NMB YAFADHILI MAONYESHO YA UBUNIFU WA WATOTO

$
0
0
Benkiya NMB imefadhili maonyesho ya ubunifu wa watoto waliokusanywa na Tanzania Mitindo House, maonyesho ambayo yatahusisha shughuli mbalimbali za kazi za mikono ambazo watoto wenye vipaji wamekua wakizifanya.
Maonyesho haya yataanza tarehe  8 Juni hadi tarehe 9 juni 2013 kuanziasaa 9 hadisaa 2 usiku pale Tanzania Mitindo House. Kwa msaada wa benki ya NMB, watoto hawa watauza kazi zao na kujipatia fedha ambazo zitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao za NMB. Fedha hizi zitawasaidia watoto hawa katika kuendeleza maisha yao ya kila siku hasa kielimu.
Tanzania Mitindo House ni Taasisi isiyo ya kiserikali ambayo imedhamiria kukusanya na kuendeleza Vipaji vya watoto yatima ambavyo vingedidimia bila msaada wowote.
Watoto hawa wanawakaribisha watu wote waweze kutembelea maonyesho ya kazi za mikono yao.
Mtoto Ahmed kutoka shule ya wasiosikia Buguruni kutoka nyumba ya watotoYatima Tanzania Mitindo House akionyesha ubunifu wa kazi yake wakati wa masomo ya kazi za mikono.
Mtoto Frank kutoka nyumba ya watoto Yatima Tanzania Mitindo House akionyesha umahiri wa kuchanganya rangi katika michoro tofauti tofauti. Frank anauwezo wa kuona lakini hana uwezo wa kusikia vizuri ni mtoto mwenye kipaji ajabu.

AMIN: BAADA YA TUZO ZA KILI NAACHIA NGOMA YANGU MPYA

$
0
0
Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (THT), Amin Mwinyimkuu ‘Amin’ amesema anasubiri tuzo zitolewe kwa wasanii ambao wameingia kwenye kinyang’anyiro cha Kilimanjaro Music ili aweze kuachia ngoma yake mpya.

Wasanii kutoka THT ambao wameingia kwenye tuzo mwaka huu ni pamoja na Barnaba, Linnah, Recho, Ally Nipishe na Makomandoo.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Amin alisema kwasasa hawezi kuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nipoze roho’ kutokana na kwamba wapenzi wa muziki huo kwasasa watakua bize na upigaji kura.

“Kwasasa mashabiki hawataangalia kitu kipya, wengi wanataka kujua msanii gani kashinda kwenye kinyang’anyiro gani na sio kuangalia msanii yupi katoa wimbo mpya,” alisema Amin.

Amin aliwataka wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kukipokea kibao hicho ambacho anaamini kitaanza kusikika baada ya kumalizika kwa tuzo hizo.

Amin kwasasa anatamba na kibao chake cha ‘Ni wewe’ ambacho kinafanya vizuri katika tasnia hiyo.


JOA KASSIM AGEUKIA TASNIA YA FILAMU

$
0
0
Na Elizabeth John


MWANADADA anayeng’ara katika tasnia ya muziki wa taarabu, Joah Kassim kutoka kundi la T-Moto amesema amegeukia tasnia ya filamu ili kuonesha kipaji chake kwa mashabiki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Joah alisema ameamua kufanya hivyo ili kuonesha kipaji chake na kwamba yeye ni msanii anajua nini anachokifanya katika fani hizo ambazo anauhakika anafanya vitu ambavyo vinapendwa na jamii.

“Mimi kama msanii anatakiwa kuonesha kipaji changu, filamu hii ni ya kwanza kucheza, nimecheza na mhogo mchungu, najua wasanii wa filamu wakiiona hii watanitafuta kutaka nicheze filamu zao, nina uhakika na nilichokifanya ndani yake,” alisema.

Joah aliwataka wapenzi wa filamu nchini, kumpokea vizuri katika tasnia hiyo pamoja na kumpa sapoti katika kazi zake.


Kundi la T-Moto Taarabu kwasasa wanatamba na kibao chao cha ‘Domo la Udaku’ ambacho kinafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo na pia wanajiandaa kukamilisha kazi yao mpya inayojulikana kwa jina la ‘Kuna mungu sio miungu’.

CHANETA WAMPATA KATIBU MKUU

$
0
0
Na Elizabeth John
CHAMA cha Netibali Tanzania (CHANETA), kimemteua Katibu Mkuu wa muda, Dk. Maimuna Mrisha ambaye atafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya chama hicho kwa kipindi cha miezi sita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHANETA, Annie Kibira, alisema katika kikao kilichowakutanisha kamati ya utendaji Juni Mosi walimteua katibu hiyo ambaye watafanya kazi pamoja hadi Desemba mwaka huu.

Aidha, Kibira alizitaka timu ambazo zitashiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki, kuthibitisha na kukamilisha taratibu zote kabla ya Juni 10.

“Klabu ambazo zitashiriki michuano hiyo ambayo itafanyika Nairobi Kenya, kuanzia Julai 13 hadi 20 ni Filbert Bayi, JKT Mbweni na Jeshi Stars,” alisema.

Mbali na hayo, Kibira alisema Jini 2 CHANETA na CHANEZA walikutana kisiwani Zanzibar, wajumbe 20 walihudhulia kikao hicho ambapo makubaliano na maazimio ya pamoja yalipitishwa kwa utekelezaji.

Kibira alitaja mambo ambayo yalijadiliwa katika kikao hicho na yanatakiwa kufanyiwa kazi na vyama hivyo kuwa ni pamoja na Utambulisho wa vyama kimataifa, Uwakilishi katika mikutano ya kimataifa, Mawasiliano na vyama vya kimataifa, Aina ya mashindano ya kimataifa yanayohitaji ushiriki wa pamoja.

Mengine ni mafunzo ya ndani na ya kimataifa, mafunzo ya kimataifa nje ya nchi, Ada za vyama kwa ulipaji wa pamoja, Miradi ya pamoja, Misaada ya kutosha kutoka vyama vya kimataifa, Uteuzi wa mwalimu wa timu za taifa za muungano, Uteuzi wa viongozi wa timu za taifa za muungano, Uteuzi wa timu za taifa za muungano, Ulipaji wa gharama za timu za taifa na muungano.

Mengine ni Ulipaji wa gharama za walimu na viongozi wa timu za taifa za muungano, Mawasiliano baina ya CHANETA na CHANEZA, Usimamizi na utekelezaji wa makubaliano, pamoja na Marekebisho ya makubaliano.


Aliongeza kuwa makampuni au taasisi zinakaribishwa kutumia mchezo wa Netiboli kutangaza bidhaa na huduma zao ikiwa ni pamoja na kujenga viwanja vya mchezo huo.

RAIS AZUNGUMZA NA BALOZI WA OMAN NCHINI

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maapinduzi DK. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Yahya Moosa  Albakri, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar Leo asubuhi kwa mazungumzo. (Picha na Ramadhan Othman Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maapinduzi DK. Ali Mohamed Shein,akizungumza na   Balozi wa Oman Nchini Tanzania  Yahya Moosa  Albakri,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar Leo. asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maapinduzi DK. Ali Mohamed Shein,akifuatana na  Balozi wa Oman Nchini Tanzania  Yahya Moosa  Albakri,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar Leo asubuhi,baada ya mazungumzo yao.

UCHAGUZI MKUU BFT JULAI 7

$
0
0
Na Elizabeth John
SHIRIKISHO la ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) linatarajia kufanya uchaguzi wake Mkuu Julai 7 mwaka huu jijini Mwanza baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema nafasi ambazo zitagombewa ni Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Mweka Hazina na nafasi tisa za  wajumbe.

Mashaga alisema fomu zilianza kutolewa Juni 4 katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT)na kwamba usaili kwa wagombea wote utafanyika Julai 5 jijini Mwanza.

Alisema gharama za fomu hizo kwa wagombea ni sh. 150,000 nafasi ya Rais, sh. 100,000 kwanafasi ya Makamu wa Rais, Katibu Mkuu na Mweka Hazina, sh. 50,000 kwa wajumbe.


Aliongeza kuwa Shirikisho linatoa wito kwa watanzania wenye uwezo wa kuongoza michezo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo kwa miaka mine ijayo.

MASHINDANO YA RIADHA YA TAIFA YAPIGWA KALENDA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

BAADA ya Zanzibar kujitoa kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana ya riadha ya kanda ‘Eastern Regional Jr Championship’ hatimaye mashindano hayo yamepigwa kalenda hadi Juni 13 mwaka huu ambapo yatafanyika jijini Dar es Salaam.

Tanzania ilikuwa imepewa uenyeji wa mashindano hayo, ambapo Chama cha Riadha Tanzania (RT), kikaipa Zanzibar; mashindani ambayo yalikuwa yafanyike Juni 8 na 9 kwenye Uwanja wa Amani, lakini kwa sasa yatafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini humo.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa RT, Mujaya Suleiman Nyambui, alisema mashindano hayo yatakayoshirikisha nchi 10 yamesogezwa mbele kutokana na mabadiriko hayo yaliyojitokeza.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na tunaamini maandalizi yataenda vizuri ili mashindano yafanyike kama yalivyo pangwa” alisema Nyambui.

Alisema nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ni Kenya, Uganda, Somalia, Misri, Eritrea, Ethiopia, Djibouti, Sudan, Zanzibar na wenyeji Tanzania.

MEZ B: SITAMSAHAU ALBERT MANGWEA

$
0
0
Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Moses Bushamaga, amesema hawezi kumsahau msanii mwezie marehemu Albart Mangweha ‘Ngwea’ kutokana na kuwa na ushirikiano mzuri na wenzie anapokuwa kazini.

Akizungumza na Habari Mseto, Mez B alisema Ngwea alikuwa ni msanii ambaye anajua nini anachokifanya katika tasnia hiyo, pia alikuwa anaonesha ushirikiano wa kutosha kwa wasanii wenzie.

“Kiukweli Ngwea hakuwa kama wasanii wengi wa kisasa kwamba kuwabagua wenzie na kujiona yeye ndio staa, yeye alikuwa anaona wote wapo sawa na wapo kwa ajili ya kutafuta na sio majungu,” alisema Mez B.

ZIJUE JEZI MPYA KWA KLABU ZA LIGI KUU YA ENGLAND 2013/14

$
0
0

LONDON, England


WAKATI maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya England 'Barclays Premier League' yakishika kasi, klabu za ligi hiyo ziko katika hekaheka kali na ya aina yake ya kutambulisha jezi mpya za vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao ambao utaanza katikati ya Agosti, huku Man United ikiwa bingwa mtetezi.


Habari Mseto Blog inazileta kwako msomaji wake aina mpya ya jezi za timu mbalimbali kwa ajili ya msimu ujao, ambapo chache zimefanya marekebisho makubwa na nyingine mabadiliko madogo katika jezi hizo kwa ajili ya Ligi Kuu msimu wa 2013/14.

Fuatana na Habari Mseto Blog kutambua aina hizo na maelezo yake kwa ufupi:
Cardiff City
Vivid: Puma unveiled their new Cardiff City home strip for the club's maiden Premier League season on Wednesday, though fans were quick to criticise the two-tone red colour
Jezi zilizotengenezwa na Kampuni ya Puma zitakazovaliwa na timu ya Cardiff City itakapocheza dimba la nyumbani za msimu wa Ligi Kuu. Cardiff City ni kati ya timu tatu zilizopanda daraja.
Chelsea
True Blues: David Luiz, Gary Cahill, Fernando Torres and Oscar model the new Chelsea kit
'True Blues' David Luiz, Gary Cahill, Fernando Torres na Oscar wakionesha jezi za Chelsea msimu ujao.
juan mata
Petr Cech
Kutoka juu ni Juan Mata, Petr Cech, Fernando Torres na Oscar wakionesha jezi za msimu ujao za Chelsea.
Fernando Torres
Oscar
Oscar akiwa ndani ya jezi mpya za Chelsea.
All white on the night: Chelsea's Adidas away strip is simple but attractive
Jezi mpya za Chelsea zitakavyokuwa msimu ujao. Zimetengenezwa na Kampuni ya Adidas.
Chelsea away strip promotional poster
Juan Mata na David Luiz wakionesha jezi mpya za Chelsea msimu ujao.
Liverpool
Staying put? Luis Suarez posed in the new Liverpool strip alongside Steven Gerrard and Pepe Reina
Mshambuliaji Luis Suarez akipozi ndani ya uzi mpya wa Liverpool. Wengine ni Steven Gerrard na Pepe Reina.
Past glories: The kit takes inspiration from the strip worn by the European Cup winning side of 1984
Past glories: The kit takes inspiration from the strip worn by the European Cup winning side of 1984
Muonekano wa eneo la shingoni katika jezi mpya za Liverpool, ambazo zinafanana kwa kiasi kikubwa na zile za mwaka 1984 walizotwalia ubingwa wa Ulaya.
Past glories: The kit takes inspiration from the strip worn by the European Cup winning side of 1984
Past glories: The kit takes inspiration from the strip worn by the European Cup winning side of 1984
Jezi ya nyumbani ya Majogoo wa Jiji Liverpool kwa ajili ya msimu ujao.
Not good: Steven Gerrard, Pepe Reina and Luis Suarez model the new Warrior Liverpool away strip
Steven Gerrard, Pepe Reina na Luis Suarez wakionesha jezi za ugenini za Liverpool aka Wekundu wa Anfield.
Not good: Steven Gerrard, Pepe Reina and Luis Suarez model the new Warrior Liverpool away strip
Jezi mpya za Liverpool. Kutoka kulia ni Danny Sturridge, Steven Gerrard, Pepe Reina na Andy Johnson.
Manchester City
Trim: The sky-blue jersey is complete with a navy and white lining
Jezi mpya za Man City itakavyokuwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya England.
Watch and learn, Gael: Milner shows his prowess as Clichy watches
Gael Clichy kulia akiwa na James Milner wakionesha jezi mpya za Man City.
Samir Nasri
James Milner
Samir Nasri juu na James Milner chini wakionesha jezi mpya za Man City msimu ujao wa 2013/14.
Glimpse: Joe Hart
Joe Hart
Mlinda mlango wa Manchester City, Joe Hart akionesha jezi mpya za klabu yake. 
Manchester United
New era: Manchester United will enter a new chapter under David Moyes in this classic Nike home shirt
Jezi mpya za nyumbani Old Trafford zitakazovaliwa na Man United msimu ujao wa Ligi Kuu ya England.
New era: Manchester United will enter a new chapter under David Moyes in this classic Nike home shirt
New era: Manchester United will enter a new chapter under David Moyes in this classic Nike home shirt
New era: Manchester United will enter a new chapter under David Moyes in this classic Nike home shirt
New era: Manchester United will enter a new chapter under David Moyes in this classic Nike home shirt
Juu inaonesha muundo wa 'collar' ya jezi mpya ya Man United msimu ujao, ambayo ina kifungo kimoja nyuma (kama kinavyoonekana) na vifungo viwili kwa mbele vya kuibana 'collar' (kama inavyoonekana) picha ya chini.
Newcastle United
New design: Steven Taylor shows off Newcastle's latest away kit
Nyota Steven Taylor akionesha jezi za Newcastle United zitakazotumiwa msimu ujao katika mechi za ugenini.
Norwich City
Game for a laugh: Bradley Johnson, Robert Snodgrass, Russell Martin and John Ruddy challenge the youngsters (below) to a game
Wachezaji wa Norwich City Bradley Johnson, Robert Snodgrass, Russell Martin na John Ruddy wakiwa ndani ya uzi mpya wa kikosi chao msimu ujao.
Game for a laugh: Bradley Johnson, Robert Snodgrass, Russell Martin and John Ruddy challenge the youngsters (below) to a game
Vijana waokota mipira 'Ball Boys' wa Norwich City wakiwa ndani ya uzi mpya utakaotumiwa na timu yao msimu ujao.
Stoke City
Striking: Peter Crouch and Robert Huth in Stoke's new away kit
Kushoto ni Peter Crouch akiwa na Robert Huth wakionesha jezi za msimu ujao za kikosi cha Stoke City.
Swansea City
Classic: Simple lines and a v-shaped neck feature on the new Adidas Swansea City home shirt
Mfano wa jezi ya msimu ujao itakayotumiwa na kikosi cha Swansea City iliyotengenezwa na Kampuni ya Adidas.
West Ham United
Hammer time: Matt Jarvis (left) sports the new West Ham home kit, while Kevin Nolan wears the away shirt
Kushoto ni Matt Jarvis akiwa na jezi ya nyumbani ya West Ham United msimu ujao na kulia ni Kevin Nolan akiwa na jezi za ugeniniza Wagonga Nyundo hao wa jiji la London.

AFRICA BARIC GOLD WAIFWAGIA FEDHA REDD'S MISS MARA 2013

$
0
0
Ofisa kutoka kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Barrick Gold Mining Fatuma Mssumi akimkabidhi Kaimu Ofisa Tawala wa Mkoa wa Mara mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni hiyo kwenye mashindano la Redd's Miss Mara yatakayofanyika leo mjini Musoma.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd's Miss Mara 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jana ikiwa ni siku moja kabla ya warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.
 Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Mara 2013 wakiwa wenye furaha.
Baadhi ya warembo wakiwa katika pozi
Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd's Miss Mara 2013 wakitembea kwa pamoja leo ikiwa ni siku moja kabla ya warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.

KHADIJA KOPA AFIWA NA MUME WAKE

$
0
0


 Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kuapanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa leo. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya (kushoto) akimfariji msanii na taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leoa alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.

PICHA ZA VITABU DHAIFU VYA ELIMU

$
0
0
 Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), akionesha makosa yaliyomo kwenye vitabu vya shule za msingi kwa waandishi wa habari mjini Dodoma. Vitabu hivyo viliidhinishwa na EMAC bila kubaini kasoro hizo. Kushoto ni, David Kafulila na Felix Mkosamali. (Picha na Edson Kamukara)
 Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), akionesha makosa yaliyomo kwenye vitabu vya shule za msingi kwa waandishi wa habari mjini Dodoma jana. Vitabu hivyo viliidhinishwa na EMAC bila kubaini kasoro hizo. (Picha na Edson Kamukara)
Vitabu vya shule ya msingi vilivyoandikwa kimakosa mathalani hiki cha Jiografia darasa la sita kinasomeka Jografia

WENGI WAJITOKEZA MAZISHI YA MANGWEA

$
0
0
 Mwili ukiwasili katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Umati wa watu wakiwa nje ya Uwanja wa Jamhuri wakati wa kutoa heshima za mwisho.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akimfariji mama mzazi wa marehemu, Albert Mangwea.
 Waombolezaji walishindwaji kujizuia.
 Mbunge wa Mbeya, mjini Joseph Mbilinyi akitoa heshima za mwisho.
 Waombolezaji wakishusha jeneza lililokuwa na mwili wa msanii mahiri wa Hip Hop, marehemu Albert Mangwea, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika mjini Morogoro leo
 Jeneza likishushwa kaburini.
Waombolezaji wakishusha jeneza lililokuwa na mwili wa msanii mahiri wa Hip Hop, marehemu Albert Mangwea, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika mjini Morogoro leo.

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KITUO CHA KUREKEBISHA TABIA KWA WANAWAKE NA WASICHANA WATUKUTU CHA PERTAPIS HUKO SINGAPORE

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa msichana anayetunzwa katika kituo cha watoto wa kike watukutu cha Pertapis kilichoko Singapore wakati alipokitembelea kituo hicho. Mama Salma yupo nchini Singapore akiambatana na Rais Kikwete katika ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo. Kulia ni Mkuu wa kituo hicho Mama Sahnim Sokaimi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na uongozi wa kituo cha kuwatunza wasichana na wanawake watukutu cha Pertapis kilichoko nchini Singapore.
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati yake na uongozi wa kituo cha kuwarekebisha tabia wanawake na wasichana cha Pertapis kilichoko huko Singapore wakati alipokitembelea. Kushoto kwa Mama Salma ni Mama Badriya Kiondo, Afisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India.  
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati yake na uongozi wa kituo cha kuwarekebisha tabia wanawake na wasichana cha Pertapis kilichoko huko Singapore wakati alipokitembelea. Kushoto kwa Mama Salma ni Mama Badriya Kiondo, Afisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India.  
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa somo kwa wasichana watukutu wanaotunzwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia zao cha Pertapis kilichoko jijini Singapore wakati alipokitembelea.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa somo kwa wasichana watukutu wanaotunzwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia zao cha Pertapis kilichoko jijini Singapore wakati alipokitembelea.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mama Sahnim Sokaimi, Mkuu wa kituo cha kurekebisha tabia za wanawake na wasichana watukutu cha Pertapis kilichoko nchini Singapore mara baada ya kukitembelea.(PICHA NA JOHN LUKUWI).

NANI KUMRITHI MISS TANZANIA BRIGIT ALFRED TAJI LA REDD'S MISS SINZA?

$
0
0
Warembo 11 kati ya 12 wanaopanda jukwaani leo kuwania Taji lenye Sifa Kuu mbili ya Redd's Miss Sinza 2013, lakini pia linaloshikiliwa na Redd's Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred, leo katika Ukumbi wa Meeda Club uliopo Sinza Mori. Katika shindano hilo litakalosindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa Bendi mahiri ya African Stars, 'Twanga Pepeta', viingilii vitakuwa ni Sh. 20,000/= kwa VIP na Sh. 10,000/= kwa viti vya kawaida. Shindano hili limedhaminiwa na Redds Original, Mtandao wa Sufianimafoto Blog, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group na Salut5.com.
Mshiriki mwenye No, 9-Sarahy Paul (23)..
Mshiriki mwenye No 8-Happyness Maira (19)
Mshiriki mwenye No, 11-Nicole Michael (21)
Mshiriki mwenye No, 5-Presca Element (20)
Mshiriki mwenye No, 3-Maua Abdul (18)
Mshiriki mwenye No, 7- Agnes Simon (22)
Mshiriki mwenye No, 1-Catrina Laurence (19)
 Mshiriki mwenye No, 6-Jacqueline Robert (20)
 Mshiriki mwenye No, 4-Doris Mwaipopo (19) 

Mshiriki mwenye No, 10-Martha Joseph (19)
 Mshiriki mwenye No, 2-Nasra Hassan (18)
 Mwalimu wa warembo hao, Mwajay Model, akionyesha uwezo wa kusebeneka, wakati akifungua rasmi shoo ya warembo hao ya kujitambulisha katika Promosheni maalum ya utambulisho wa shindano lao iliyoandaliwa na kinywaji cha Redd's katika Baa ya Mary Land Mwenge jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni mshereheshaji wa hafla hiyo fupi..... 

Warembo hao wakipozi kusubiri utaratibu baada ya kuwasili eneo la tukio jana usiku.

Warembo wakimshangilia mwenzao wakati akipita mbele kwenda kujitambulisha, ''sasa sijui na leo jioni huyu ndiye atakayeshangiliwa kama hivi?''

Mwalimu wa warembo hao, Majay (kulia) akipozi na warembo wake.

Hapa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao ya maandalizi.

Mil. 16/- za MKUKUTA zahujumiwa Mvomero

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mvomero
MILIONI 16,076, 2240/- za Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) zilizogawiwa na Halmashauri ya Mvomero kwa Kata ya Mhonda, zinawapa wehu watendaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Kiongozi mmoja akituhumiwa kuanza kuzihujumu.
Hujuma hiyo imebainika Juni 6, 2013 ambapo Wajumbe 21 wa CCM wa Halmashauri ya Kijiji cha Kichangani kilichogawiwa na Halmashauri ya Wilaya Mvomero Mil. 7,562,169/-, kutishia kujiuzulu na ikibidi kujiunga na vyama vingine, baada ya Kiongozi huyo kutoa Hundi la Mil. 2.5/-.
Mgao wa fedha hizo zinazowapa wehu watendaji hao kiasi cha CCM kukiondolea kukubarika zimegawanywa Vijiji Vitano na kiasi chake kwenye Mabano. Kichangani (Mil. 7,562,169/), Hubiri (1,332,855/-), Mafuta (Mil.1, 193,012/-), Mhonda (3,471,982/-) na Kwelukwiji (Mil.2, 516,222/-).
“Baada ya kuparangana na kutoafikiana na Hundi ya Mi.2,5/- iliyotolewa na Kiongozi wa Kata kwa Kijiji chetu cha Kichangani, alimpigia Simu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mvomero Jonas Van Zealand, na alipofika aliamuru mgao wetu tupewe kama ulivyo”.alisema mtoa habari toka ndani ya Kikao.
Tanzania Daima liliongea na wananchi na baadhi ya Viongozi wa Vijiji wa Kichangani, Hubiri, Mafuta, Mhonda na Kwelukwiji kwa nyakati tofauti, ambapo wote walielezea kutokuwa na Imani na Kiongozi huyo wa Kata Jina linahifadhiwa, kwa madai kwamba hana Uadilifu, na kwamba inasemekana amejilipa Mi. 1.5/- anazodia alikikopesha Kijiji cha Kichangani, jambo linapingwa.
“Alikikopesha Kijiji kama Nani? Nani aliyemruhusu ajilipe na kuna Makubaliano gani hadi afanye hivyo bila ya ridhaa ya sisi wananchi? Kama Mwenyekiti wa Halmashauri hatamuwajibisha au kujiuzulu mwenyewe, ambaye ameshuhudia Kosa alilofanya. Tutahamasisha kumng’oa”.Mjumbe mmoja akisema wameacha kujiuzulu sababu ya Ombi la Zealand.

Aidha hadi tunakwenda mitamboni, Zealand alipotafutwa kwenye Simu yake ya Kiganjani 0718132507 kuzungumzia tukio hilo ilikuwa imefungwa, ambapo pia Diwani wa Kata ya Mhonda Salum Mzugi 0658292149, naye hakupatikana. Ila Diwani Viti Maalum Juliana Petrol (Chadema) alisema alisafiri hivyo atalifuatilia. Na ikibainika Chama chake hakina kulala. Lakini wananchi wamesema wana Imani Zealand atalishughulikia.

WASHINDI WA SHINDANO LA 'TWITI' WAZO JIPYA KUONDOA UMASIKINI WAPEWA ZAWADI ZAO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi shindano la Twiti Wazo Jipya Kuondoa Umaskini jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dk. Donath Olomi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi kitita cha sh. milioni 1 mshindi wa kwanza wa shindano la  Twiti Wazo Jipya Kuondoa Umaskini, Jilly Gaudence Kyomo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dk. Donath Olomi. Kulia ni mshindi wa pili, Peter George na mwanafunzi wa chuo cha CBE, Ludovick Angelino.
 Mshindi wa pili, Peter George akipokea kitita cha sh. laki 5
Mshindi wa tatu akipokea kitita cha sh. laki 3.

Na Mwandishi Wetu

VIJANA watatu wa jijini Dar es Salaam, wameibuka washindi katika shindano la Dk. Reginald Mengi la ‘Kutwit’ kuondoa umasikini nchini.

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo lililopewa jina la Twiti Wazo Jipya Kuondoa Umasikini ni Jilly …. ambaye aliibuka na kitita cha sh milioni moja, Peter George (sh 500,000) na Ludovick Angelino (300,000).

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya IPP, Dk. Mengi alisema shindano hilo lina lengo la kuibua mawazo mapya jinsi ya kupambana na umasikini.

Alisema washiriki wa shindano hilo lililozinduliwa Mei 13 na washiriki wengi walijitokeza kuibua mawazo mapya na washiriki watatu ndio walioshinda.

Dk. Mengi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, alisema mchakato wa kupata washindi, ulisimamiwa na Kiongozi wa Taasisi ya Chuo cha Uongozi na Ujasiliamali (IMED), Donath Olomi na jopo lake.

Akizungumza jinsi washindi hao walivyopatikana, Dk. Olomi alisema jumla ya Twits 481 zimepokelewa kati ya Mei 13 hadi 31.

Alisema vigezo vilivyotumika katika mchakato huo ni wazo lililoeleweka  na kuelezeka kirahisi,  lisiwe wazo ambalo limeshasikika mara nyingi na liwe linaweza kutekelezeka.


Alisema mshindi wa kwanza Jilly alitoa wazo lililosema ‘Tuwe na utamaduni wa kupenda kile tukifanyacho, tukifanya kwa moyo, uadilif, heshima na kujali muda hata kama it’s self employed. 
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>