Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Nchi hii,Watuhumiwa Waharifu Wanapongezwa?

$
0
0
Na Bryceson Mathias
KATIKA Serikali ya aina yoyote duniani, Jamii, Madhehebu ya Dini, Asasi za Kiraia na Vyombo mbalimbali vya kutetea Haki za binadamu, hakuna anayeweza kumpongeza au kumtunuku mtu ambaye anatuhumiwa kufanya Uharifu.
Hatua hiyo haifikiwi hivyo kwa sababu, Pongezi hutolewa kwa mtu, Kikundi au Taasisi ambayo imefanya vizuri katika utendaji wake kutokana na Ueledi, Uadilifu na Uwajibikaji wa kile anachokifanya, anachokiongoza, na kukitekeleza kwa wakati muafaka na gharama nafuu.
Lakini katika siku za hivi karibuni, wananchi waliohojiwa kwa nyakati tofauti, wameanza kushangazwa kuona kwamba, kuna watu miongoni mwetu wanapata Tuzo za aina mbalimbali, Ijapokuwa, wengi wanaopongezwa, wana tuhuma za uharifu.
Nyakati hizi, Utashangaa Mtu au Mfanyakazi Umma, anafanya ubadhirifu mkubwa wa fedha au Rasilimali za Umma katika sehemu ya Kazi, lakini atapewa Tuzo, Cheo au Uhamisho kwenda sehemu nyingine ili akaharibu na huko, Ingawa uovu wake unafahamika.
Mtu akiharibu na kufuja mali ya Umma na kumhamishia mahali pengine, ni sawa sawa na kumtunuku Cheo au kumpongeza kwa alichoharifu, Jambo ambalo wengi wa wananchi wanahoji Je, anapongezwa kwa Uharifu ule aliofanya ili aendelee kufanya?.
Mfano; wananchi wanasema baadhi ya Wakurugenzi wa Wilaya nchini, wamebainika na Ofisi ya Ukaguzi wa Serikali nchini (CAG), kwamba wamefuja au kulipa Wakandarasi malipo hewa kwa kazi ambazo hawakufanya, na kukataliwa na Mabaraza ya Madiwani wao.
Lakini cha kusikitisha, badala ya kuchukua hatua na kutakiwa kurejesha au kulipa walichoharifu, wamepata tuzo za pongezi au vyeo ili waendeleze kuliharifu Taifa kwa Tabia zao zinazohojiwa na wananchi.
Katika Wilaya ya Mkulanga kwa mfano; baadhi ya Walimu wamelalamikia Kitendo cha Walimu wenzao wawili, waliokuwa Wakuu wa Shule za Sekondari, na kufuja Mamilioni ya Fedha za Ujenzi wa Nyumba za Walimu, Ada na Michango ya Serikali, kuhamishiwa Shule zingine.
Pia wamelalamikia Upendeleo uliofanywa kwa Walimu wenye Makosa hayo hayo kupewa adhabu mbili, kushushwa Ualimu Mkuu na kuwa Walimu wa Kawaida, wakifuatiwa na Uhamisho kwenda Mahali pengine. Je tuna sababu ya kuwapongeza waharifu hao?
Kufafanua Malalamiko hayo yanayoainisha karibu Mil. 66/- zimetumiwa vibaya katika Ujenzi wa Nyumba za Walimu, Mkurugenzi Wilaya ya Mkulanga, Saada Mwaluka, alisema, Mimi ni Mgeni wilayani hivyo sifahamu chochote kuhusu madai hayo, Ila nitafuatilia”.
Afisa Elimu Vifaa wa Wilaya, Mussa Ally, alipohojiwa na Mwandishi wa Makala hii, alikanusaha kupotea Mil. Sita kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Walimu pekee, ila alikiri fedha hizo ni za Ujenzi wa Nyumba za Walimu, Ada na Michango mbalimbali.
Kuhusu kushushwa Vyeo kwa Walimu na Uhamisho uliofanyika, alidai unatokana na Waliokaimu nafasi hizo kushindwa kuonesha Uwezo wao na mashirikiano na Halmashauri, ambapo kila mmoja wao ana Jambo la kujibu kutokana na Wakaguzi kutaka wajibu hoja.
Hivi karibuni Kamanda wa Polisi Iringa, Michael Kamuhanda, alipandishwa Cheo ingawa alilalamikiwa sana na kutuhumiwa kupelekea Mauaji ya Daudi Mwangosi. Pamoja malalamiko hayo, amepandishwa Cheo pamoja na Tuhuma alizotuhumiwa.
Aidha katika Biblia Takatifu Mungu anasema hivi, “Mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali. Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda” (2tim.2:5-6). Familia ya Mwangosi ilikuwa iwe ya kwanza kutunukiwa.


Hakimu kukosekana kwa sababu nyepesi, hatua gani zichukuliwe?

$
0
0
Na Bryceson Mathias 

KUMEKUWEPO na wimbi la baadhi ya Mahakimu, kutokuwepo mahakamani kuhukumu kesi walizopangiwa kwa mfululizo, hivyo kushindwa kuhukumu kesi na kukwamisha mwendelezo wake na watuhumiwa kurudi bila kesi zao kusikilizwa.

Hivi sasa wapo watu ambao wanateseka na kukaa gerezani kwa muda mrefu kwa sababu tu, watendaji na Hakinu hawapo, ambapo kukosekana kwao hakuoneshi mashiko zaidi ya kuwa na sababu nyepesi, na linalokwamisha kesi husika zisiendelee mahakamani.

Mahakama zimekuwa kama zinawaadhibu watu wasio na hatia! ambapo ningeitaka Mahakama na serikali kukomesha tatizo hilo na kuacha kuwaadhibu watu bila sababu! Ikibidi Hakimu asipokuwepo, awekwe Mbadala kazi iende.

Ningependa, ikitokea Hakimu hayupo, ni vizuri Uongozi wa Mahakama uweke Mbadal wake, kuliko kuacha watu wasubiri hadi wiki nyingine tena huku Watuhumiwa wakiendelea kukaa mahabusu bila sababu.

Sioni sababu za msingi zinazosababisha kesi zisizohitaji uchunguzi ambazo uchunguzi wake umekamilika kutotolewa uamuzi haraka, hasa wakati mwingine mtu kakanyaga Nyanya au hakuvaa Kofia Gumu (Helmet), apewe Faini aende.

Ni rai yangu, Serikali na Wiziri ya Katiba na Sheria na Ofisi hiyo, iweke muda maalum ambapo kesi za Jinai kwa mfano, Kesi za Madai, Biashara na kadharika, ziwe na muda ambao Ukifika, lazima kesi hizo ziwe zimekwisha.

Tukifanya hivyo tutawafanya mahakimu na wanaowasaidia Polisi na Magereza, kuwajibika na kuisaidia Mahakama, kutimiza malengo yao (Tentative Time), hivyo tunaweza kupima ufanisi wa vyombo hivyo na kuvizawadia.

Ukifanye uchunguzi Magereza nyingi; Utakuta Mahabusu wengi katika Magereza, hawafikishwi Mahakamani kwa sababu ya Mahakimu na Watendaji wa Mahakama kutokuwepo kwa sababu ya Udhuru mbalimbali, na Mahakama haiweki mbadala wake.

Kwa kuendekeza kuwaweka watuhumiwa kwa muda mrefu, hasa kwa wale ambao Kesi zao ni za kudhulumiana au kuiba Njiwa, anakaa gerezani kwa Gharama ya Bajeti ya Mahakama ya Wilaya au Mkoa, ni Matumizi mabaya ya fedha.

Nafahamu kesi zikishafunguliwa mahakamani sheria na kununi za uendeshaji zinataka kesi isikilizwe na itolewa uamuzi mapema ila kama kuna sababu ya msingi inayosababisha kuchelewesha uamuzi. Lakini si kesi ya kuiba Bata ikae miaka mitatu.

Tufike mahali Serikali, Bumge na Mahakama kama vyombo muhimu (Mihimili Mitatu), watendaji wa Magereza na Polisi, waelewe Thamani ya Kodi (Value for Money) ili tuwe na tahadhari ya Gharama hizo (Cost Conscious).

Haingilii akilini kuwaweka wamachinga 100 gerezani, wakala Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya Robo mwaka, kwa kosa la kutembeza Mitumba, kosa la kuvuka na nguo kulipokuwa na msafara wa Mgeni toka nje. Huyu ni Mtanzania atembeze nguo wapi?

Wakati mwingine, kumekuwa na wingi wa kesi zinazofunguliwa unaokinzana na idadi ndogo ya watumishi waliopo kwa sababu kesi zingine ni ndogo zisizo na madhara kwa Taifa, mfano unamuweka ndani mzazi ambaye hajalipa michango ya Shule ya Msingi! Aibu.

Mashahidi kusababisha kesi kuahirishwa mara kadhaa, mahabusu kutofikishwa mahakamani, dharura kwa watendajii mahakamani, Hakimu, Mwendesha mashtaka, Wakili wa utetezi, mshtakiwa na wazee wa baraza, haya yamo ni ya uwezo wetu.

Uhamisho wa mahakimu unaosababisha kesi zisiendelee hadi atakapopatikana hakimu mwingine wa kuendelea kusikiliza kesi hiyo au kuanza upya kwa kadiri sheria itakavyohitaji kwa kesi husika ambavyo naona ni kuviendekeza, maana vinatatulika. 

Serikali yaombeleza kifo cha Mangwea

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO 


 SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA KIFO CHA
BW. ALBERT MANGWEA, (Man Ngwair)
1/06/2013.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangwea, aliyefariki huko Afrika  Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa katika shughuli za muziki, Jumanne  tarehe 28 Mei, 2013.

Kifo cha Albert Mangwea ni pigo kubwa kwa fani ya muziki hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji ya “Free Style” alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani na nje ya nchi.

Albert Mangwea atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki  kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.

 Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote  na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.

Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa  yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

“Mwenyenzi Mungu ailaze roho yaAlbert Mangwea mahala pema peponi.”

 Imetolewa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara

MKUTANO WA CCM MAKAMBAKO JIONI HII WAFANA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kimama akihutubia mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa michezo mjini Makambako mkoani Njombe.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe, Deo Sanga akitoa yake ya moyoni mbele ya wananchi kabla ya kumkaribisha Kinana kuhutubia mkutano huo.
 Ilibidi badhi ya wananchi kuongeza urefu wao kwa kusimama kwenye baiskeli kuweza kuona kila kilichokuwa kikifanyika kwenye mkutano huo
 Msimamizi wa utekelezaji wa ilani ya CCM, wilaya ya Njombe, Mkuu wa wilaya hiyo Saraha Dumba, akikimbilia jukwaani alipotambulishwa uwepo wake kwenye mkutano huo.
Baadhi ya madiwani wilayani Njombe, wakinyoosha mikono walipotambulishwa uwepo wao kwenye mkuyano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM, Edna Msigwa, alipokabidhi kadi kwa wanachama 150 wapya wa CCM katika mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe, Deo Sanga aka Jah People.

 Wanachama wapya waliopewa kadi ya Kinana, wakila kiapo
 Wanachama hao wapya wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Adbulrahman Kinana na viongozi wengine alioambatana nao kwenye mkutano huo.
 Kabla ya kuwasili kwenye Uwanja wa mkutano huo, Kinana alikagua mabanda ya maonyesho ya wajasiriamali katika wilaya ya Njombe. Hapa alikuwa alitazama mafuta yanayosindikwa na wajasiriamali hao
 Mapema Kinana alizindua Ofisi ya CCM tawi la Mizani, wilayani Njombe.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitabasam baada ya mkutano wake huo kufana vya kutosha. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

ALICE ASHINDA TAJI LA REDD'S MISS DAR CITY CENTER

$
0
0
 Mshindi wa Redd's Dar City Center, Alice Isack (katikati) akiwa na mshindi wa pili, Clarah Paul (kulia) na mshindi wa tatu, Fatma Hussein (kushoto). (Picha na Habari Mseto Blog)
 Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kushoto) akiwa na wadau wa urembo.
 Warembo walioingia katika hatua ya tano bora.
 Jaji Mkuu wa shindano hilo Wema Sepetu akiwa na majaji wenzake wakifuatilia shindano la Redd's Miss Dar City Center.
 Hoyce Temu akitoa utaratibu wa kujibu maswali.
 Meneja wa Kinywaji cha Redd's, Victoria Kimaro (shoto) akifuatilia shindano hilo.
 Wasanii wakitoa burudani.
 Wadau wakifuatilia shindano hilo.
Redd's Miss Dar City Center, Alice Issack 
Washindi wakiwa na zawadi zao.

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA JOPO LA WATAFITI WA MASUALA YA UCHUMI AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa Jopo la Watafiti wa Masuala ya Uchumi Afrika (AERC) kujadili athari za Mazingira kwa Maendeleo ya Bara la Afrika, uliofanyika Jijini Arusha leo Juni 02, 2013. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mtafiti wa Kisayansi Kutoka Mpango wa Pamoja unaohusu Sera za Kisayansi na Mabadiliko ya Tabianchi, Keneth Strzepek (kulia) na Mtafiti Mwandamizi wa Kisayansi,Adam Schlosser (katikati) baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Jopo la Watafiti wa Masuala ya Uchumi Afrika (AERC) kujadili athari za Mazingira kwa Maendeleo ya Bara la Afrika, uliofanyika Jijini Arusha leo Juni 02, 2013. Picha na OMR
 Profesa, Lemma Senbet, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Terezya Huvisa, kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Terezya Huvisa, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo waliohudhuria wakimsikiliza Makamu wa Rais.


BASATA YAANZA KUYAFANYIA KAZI MAOMBI YA WASANII

$
0
0
NaElizabeth John
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz), kesho wanatarajia kuzikutanisha taasisi mbalimbali zinazohusika na urasimishaji ili kutoa elimu kwa wasanii, wadau na wakuzaji wa sanaa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaimu katibu mkuu mtendaji wa BASATA, Godfrey  Mngereza, alisema kuwa taasisi hizo zitakutana katika ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba.
 
Mngereza alizitaja taasisi hizo ambazo zitakutana kuwa ni Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
 
  Alisema katika kuelekea urasimishaji wa sekta ya filamu na muziki ambao ulianza rasmi Januari mosi na ifikapo Julai mosi mwaka huu hakuna kazi yoyote ya filamu na muziki itakayoingia sokoni bila kuwa na stampu ya TRA.
 
  Pia aliwataka wadau wa sekta ya sanaa kupeleka michango na hoja zao ili kuleta mustakabali utakaojenga sekta ya sanaa.

KIBADENI AIUNGA MKONO SERIKALI HOFU YA KUPELEKA TIMU SUDAN

$
0
0
Na Elizabeth John
LICHA ya serikali kuingiwa na hofu ya kupeleka timu Sudan kushiriki michuano ya Kagame, Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Abdallah Kibadeni amesema anaiunga mkono na ni vema kuangalia hali ya usalama kwanza.
Mashindano hayo yanayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) yamepangwa kufanyika nchini humo kutokana na serikali yake kuhakikisha hali ya usalama kutokana na kuwa na mapigano kwa muda mrefu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kibadeni alisema timu yake inaendelea na mazoezi kama kawaida hata kama serikali itazuia timu hizo kushiriki wataendelea kujiweka sawa na michuano mingine.
“Usalama ni kitu cha kwanza alafu mambo mengine yanafuata, itakua haina maana vijana wetu waende huko afu hali ibadilike,” alisema Kibadeni.
Alisema timu inaanza mazoezi rasmi leo na amewataka wachezaji ambao wapo mbali warudi haraka ili aweze kupanga kikosi ambacho kinaelewa.
Tanzania inawakilishwa na Yanga ambao ndio bingwa mtetezi wa michuano hiyo na Simba kama bingwa wa bara msimu uliopita.
Simba iko kundi A na timu za El-Merrikh (Sudan), APR (Rwanda) na Elman (Somalia) wakati Yanga iko kundi C sambamba na Express (Uganda), Ports (Djibout) na Viatal’O (Burundi).
Michuano hiyo imekuwa ikifanyika chini ya udhamini wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye huto zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu.
 


WATATU KUIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA KUOGELEA

$
0
0
Na Elizabeth John
CHAMA cha kuogelea Tanzania (TSA) kimechagua wachezaji watatu ambao wanatarajia kuliwakilisha taifa katika mashindano ya Dunia ambayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Julai 18 hadi Agosti 5 katika mji wa Barcelona nchini Hispania.
Wachezaji hao wanatarajia kuondoka nchini, Julai 17 chini ya kocha wao, Geofrey Kimimba ambaye atasaidiana na makocha wa wachezaji wanakotoka.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TSA, Noel Kiunsi wachezaji hao ni Hilal Hilal, Ammaar Ghadiyali na Mariam Foum.
“TSA tulikutan ana kuchagua wachezaji ambao tunauhakika wataenda kuitangaza nchi yetu vizuri, hivyo tunaukhakika na wachezaji hao, tuwaombee kwa mungu wafanye vizuri,” alisema Kiunsi.
Alisema wachezaji hao pamoja na wenzao wanaendelea na mazoezi ya kujiweka sawa kwaajili ya kushiriki mashindano hayo katika bwawa la chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 

CHIKU AISAMBAZA 'SAUTI YAKE'

$
0
0
Na Elizabeth John
MWANADADA ambaye anatesa katika tasnia ya muziki wa hip hop, Chiku Keto, ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Sauti yangu’ ambao umeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Mbali na kutamba na kibao hicho, mwanadada huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Fahari ya Kusini’ ambacho kilifanya vizuri na kumuweka pazuri msanii huyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chiku aliwataka wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuzipokea kazi zake nyingine zinazofuata ikiwa ni pamoja na video ya ngoma hiyo.
“Najua kazi hii itapokelewa vizuri na mashabiki wangu, kwasababu mashairi niliyotumia ndani yake yamesimama kisanii hivyo naomba sapoti yao,” alisema Chiku.
Mwanadada huyo ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia hiyo, anaomba wapenzi wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuvipokea vitu vizuri kutoka kwake.

WAKUVWANGA AISAMBAZA ALBAMU YA 'KATO'

$
0
0
Na Elizabeth John
MSANII kutoka kundi la Orijino Komedi, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ ameachia albamu yake ya kwanza inayojulikana kwa jina la ‘Kato’ ambayo imeanza kufanya vizuri katika soko la muziki.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wakuvwanga alisema nyimbo ambazo zipo katika albamu hiyo, zimechanganyika alizoimba kwa lugha ya kinyakyusa na zingine ameimba Kiswahili.
“Mimi ni Mnyakyusa nimeamua kuimba kwa lugha hiyo ili hata wenzangu waliopo Mwakaleli waelewe nimeimba nini, naamini itafanya vizuri sokoni,” alisema Wakuvwanga.
Wakuvwanga aliwataka wadau wa muziki nchini wampokee katika tasnia hiyo na kuwaahidi kuwaletea vitu vizuri zaidi ya hivyo, mbali na kwamba yeye ni msanii wa maigizo.
Wasanii wengine ambao wanaunda kundi hilo la Orijino Komedi ni pamoja na Joti, Mpoki, Masanja, Vengu.

President Kikwete and former Japanese Prime Minister Yoshiro Mori speaks on Efforts to Fight Infectious Diseases

$
0
0
 A cross section of the participants to the high level panel on ““Accelerating the Global  Fight against Infectious Diseases,” held as TICAD V official side event in Yokohama, Japan this morning claps as President Jakaya Mrisho  Kikwete concludes his keynote address.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a high level panel on “Accelerating the Global  Fight against Infectious Diseases,” held as TICAD V official side event in Yokohama, Japan this morning.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and former Japan Prime Minister Yoshiro Mori shortly after they participated in a high level panel on” Accelerating the Global fight against Infectious Diseases,” held in Yokohama this morning. (Photos by Freddy Maro)

SALSHIA ISDORE NDIYE REDD'S MISS GEITA 2013

$
0
0
Mshindi wa taji la Redd’s Miss Geita 2013, Salshia Isidore (katikati) akiwa mwenye furaha wakati wa kupiga picha ya pamoja na warembo wqenzake Stella Magerezi (kulia) aliyeshika nafasi ya pili na Mshindi wa tatu wa shindano hilo, Nurieth Rashid. Salshia aliwashinda warembo wenzake 12 waliokuwa wakiwania taji hilo pamoja nae.
 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja.
 Wanyange walioshiriki shindano la Redd's Miss Geita 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jukwaani.
Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoani Geita, Vicky Kamata (kulia) akitoa nasaha zake kwa washindi na warembo wote walioshiriki shindano hilo.


Na Father Kidevu Blog, Geita

MREMBO Salshia Isidore amechaguliwa kuwa Redd’s Miss Geita 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 12 katika shindano lililifanyika Jumamosi  Juni 1,  kwenye ukumbi wa Desire uliopo mjini Geita.

Wengine walioingia nafasi ya tatu bora ni pamoja na Nurieth Rashid aliyeshika nafasi ya tatu na Stella Magerezi alishika nafasi ya pili.

Katika shindano hilo lililosindikizwa na burudani safi kutoka kwa msanii Baby Madaha na Bob Haisa huku mgeni rasmi akiwa ni Mbunge wa Viti Maalum wa Geita Vicky Kamata.

Washindi hao watatu watawakilisha mkoa wa Geita kwenye shindano la Kanda ya Ziwa ili kuwapata washiriki watakaoenda ngazi ya taifa.

Akizungumza na washindi pamoja na warembo wengine kwa ujumla Vicky aliitaka jamii ya watu wa Geita kuyatambua mashindano hayo kuwa ni muhimu na yanasaidia suala la ajira.

Alisema kuwa kupitia mashindano hayo kuna mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kuwa mashindano hayo ni fursa ya kuzungumza na wananchi kuielezea masuala mbalimbali ya kimaisha.

“ Najua kwa sasa hata katika Bunge hili la bajeti kuna mengi ambayo tumeyajadili na kuyapitisha kwa ajili ya vijana na hasa pia kupitia sanaa na hivyo mashindano kama haya yanahusika kabisa” alisema Vicky.

Naye mwandaji wa shindano hilo alisema kuwa washindi hao mshindi wa kwanza amepewa laki tatu, huku wa pili amepewa laki mbili na wa tatu laki tatu.

Rais Kikwete akutana na Mwenyekiti wa mambo ya nje wa bunge la Japan

$
0
0
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje ya bunge la Japan Mh.Katsyuki Kawai wakati mwenyekiti huyo alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo jijini Yokohama leo .Wengine katika picha kushoto ni Mbunge wa Nzega Dk. Hamisi Kigwangala na kulia ni Mbunge wa Kasulu mjini Mh.Moses Joseph Machali.Wabunge hao ni wajumbe walioko katika msafara wa Mheshimiwa Rais anayehudhuria Mkutano wa tano wa TICAD unaoendelea jijini Yokohama Japan. (Picha na Freddy Maro)

PAMBANO LA NSSF MEDIA ALL STARS NA WABUNGE KATIKA PICHA

$
0
0
 Wachezaji wa timu ya wanawake ya mpira wa Peter ya Media NSSF All Stars wakikaguliwa kabla ya mpambano na tinu ya Bunge ya mpira wa Peter wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma leo
 Wachezaji wa timu ya Mpira wa Pete ya Bunge wakikaguliwa kabla ya mchezo.
 Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na wachezaji wa timu ya NSSF Media All Stars kwa upande wa wanaume kabla ya mchezo kuanza dhidi ya timu ya Bunge Sports Club.
 Wachezaji wa Bunge Sports Cluba na NSSF All Stars wakisikiliza mawaiza kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa mchezo huo wa kirafiki  uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. NSSF All Stars kwa upande wa Mpira wa miguu walishinda 1-0 na kufanikiwa kunyakuwa kikombe na kwa upande wa mpira wa Pete Bunge walishinda 31-10
 Naibu Spika Job Ngugai (wa pili kulia), Mkurugenzi wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk. Ramadhan Dau (wa pili kushoto), Mbunge Urambo Magharib, Profesa Juma Kapuya (kulia), na Mbunge wa Sunve, Richard Ndassa wakifutilia mchezo mpira wa miguu katika ya NSSF Media All Stars na Bunge Sports Club 
 Nahodha wa NSSF All Star upande wa mpira wa Pete akikabidhiwa Kikombe na Naibu Spika baada ya kuwa washindi wa pili
 Nahodha wa Mpira wa Peter kwa timu ya Bunge, Mbunge wa Viti maalum (CUF), Mkiwa Kimwanga akiwa Kombe la ushindi baada ya kukabidhiwa na Naibu Spika Job Ndugai. 

Nahodha wa timua NSSF Media All Stars kwa upande wa timu mpira wa Miguu, Majuto Omari akionyesha Kombe baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau baada ya kuifunga timu ya Bunge Sports Club 1-0.
 Wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club wakishangilia baada ya timu ya mpira wa pete kuibuka na ushindi na timu ya mpira wa miguu kuibuka mshindi wa pili
 Wachezaji wa NSSF Media All Stars wakishangilia baada ya mchezo kumalizika.
Wachazaji wa NSSF Media All Stars wakicheza muziki baada ya kumalizika kwa mchezo.

Mkulanga yaomba Chadema Iwasaidie

$
0
0
Na Bryceson Mathias , aliyekuwa Mkulanga

BAADHI ya Wazazi, Walimu na Wananchi walio wengi wa Vikindu, Kisima na Tambaani Wilaya ya Mkulanga, wamekiomba Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) na viongozi wake,  kuwanusuru na dhuluma ya Zao la Korosho na Ufisadi wa Fedha za Ujenzi wa Sekondari.
Ombi hilo walililotoa June 1, mwaka huu walipozungumza na Mwandishi kwa nyakati tofauti, ambapo walitoa Kilio chao wakidai, Kutokana na kukopwa na kudhulumiwa bei ya zao lao la Korosho, hawana uhakika na maisha yao maana hakuna wa kuwatetea dhidi ya Uozo huo.
Mbali ya Kilio hicho, walisema wanakiomba Chadema na Viongozi wake, kuwatazama kwa jicho la tatu la huruma, ili wafike wilayani humo eneo la Vikindu, Kisima na Tambaani, ambako Fedha takribani Milioni 66/- za Ujenzi wa Nyumba za Walimu zimefujwa.
“Kwa hali ya Dhuluma ya Korosho zetu na Ubadhirifu wa Milioni 66/- uliofanywa na   waliokuwa walimu wakuu waliopewa Uhamisho baada ya Uchafu huo, palipofikia sasa tunahitaji msaada wa Nguvu Mbadala ya CHADEMA”.alisema Mwalimu aliyeomba asitajwe.
Pia Walimu hao wamelaani kitendo cha Walimu wenzao wawili waliotuhumiwa na Ubadhirifu wa fedha za Ujenzi wa Nyumba hizo, kushushwa Vyeo vya Ualimu Mkuu na kuhamishiwa Shule zingine, huku wengine wenye makosa hayo hayo wakiachwa na kuhamishwa vituo tu!.
Mwananchi mmoja anayetaka Mabadiliko ili wakulima wa Korosho wasifanywe watumwa wa kuwazalisha Korosho na wengine wafaidi na kuomba pia asitajwe alidai, kunahitajika Mapinduzi makubwa ya mabadiliko ili watu wafikie mahali pa kupata Haki inayominywa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkulanga, Saada Mwaluka, alisema “Mimi ni Mgeni wilayani, hivyo sifahamu chochote kuhusu madai hayo, Ila nitafuatilia”.  
Afisa Elimu Vifaa na Vielelezo (W), Mussa Ally, alikanusaha kufujwa Mil. 66/- za ujenzi za Nyumba za Walimu pekee, ila alikiri fedha hizo ni za Ujenzi wa Nyumba za Walimu, Ada na Michango, na kusema wahusika wana tuhuma za kujibu Hoja za Wakaguzi wa Ndani.
Aidha Kuhusu kushushwa Vyeo kwa baadhi ya Walimu na Uhamisho uliotolewa kwa upendeleo alidai,
“Unatokana na Walimu hao kukaimu nafasi hizo, ambapo walionekana wameshindwa kuonesha Uwezo wao wa Kitaaluma, Ushirikiano na Halmashauri, ambapo kila mmoja wao anatakiwa kujibu hoja (Query) za Wakaguzi, pale ambapo vithibitisho vya hati za malipo ya Ujenzi huo vilikosekana”.alisema Ally.

MAGUFULI ATAKIWA KUSAFISHA TANROAD

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ujenzi John Magufuli, ametakiwa kukomesha vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wasiowaaminifu wa Mamlaka ya Barabara Tanzania (TANROADS), vya kuuza maeneo ya hifadhi ya barabara kwa wafanyabishara kinyume cha sheria.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Diwani wa Kata ya Saranda, Efraim Kinyafu alisema watendaji hao wamejihusisha na vitendo hivyo katika maeneo ambayo yametakiwa kuwa wazi kwa ajili ya upanuzi wa Barabara Kimara hadi Mbezi.

Alisema vitendo hivyo vinavyofanywa na watendaji hao vya uuzaji wa maeneo hayo, wakishirikiana na wenyeviti wa Serikali za Mitaa vimekuwa vikisababishia hasara kw wafanyabiashara pamoja na watu wengine mara sheria inapofuata mkondo wake.

Kinyafu alisema baadhiya wafanyabiashara walioangukia kwenye mtego huo ni wale waliondolewa kwenye maeneo ya Suka na Stop Over ambao baadhi yao wameuziwa ama wamepewa maeneo mengine kinyemela kwa maslahi ya genge la walanguzi, bado kisheri hayaruhusiwi kuendesha shughuli zozote za kibinadamu.

“Kwa mfano kuna tukio la wakazi wa Kimara ambao waliuziwa eneo la hifadhi ya barabara kinyemela na watendaji hao, kwa ajili ya ujenzi Msikiti kitendo ambacho baadaye kimeleta mtafaruku baada ya msikiti huo kutakiwa kubomolewa kwa kuwa ulijengwa kwenye hifadhi ya barabara”alisema Kinyafu.

Akizungumzia mgogoro uliyozuka kati ya wafanyabiashara hao wa Kimara na TANROADS, pale walipotakiwa kuondoka pembezoni mwa barabara ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, Kinyafu alisema kwa kiasi kikubwa mgogoro huo ulichangiwa na uzembe wa wenyeviti wa serikali za mitaa kutokana na kuchelewesha barua zilizokuwa zikiwataka wafanyabiashara hao kuondoka kwa zaidi ya wiki tatu.

Alisema baada ya TANROADS kuamini kuwa barua hizo ziliwafikia wafanyabiashara hao, ilifika katika eneo husika kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa barabara hata hivyo ilishangazwa ilipowakuta wakiwa bado wapo hivyo kutokuwa na njia nyingine zaidi ya kubomoa vibanda vyao hali iliyozusha mtafaruku.


Aidha, Kinyafu aliitaka serikali kuhakikisha inawatafutia maeneo ya kudumu wafanyabiashara hao ili kuepuka misuguano ya mara kwa mara isiyokuwa na sababu, na endapo watashindwa kufanya hivyo atawaagiza wandelee kufanya biashara zao katika maeneo wanayodhani wanaweza kujipatia wateja kirahizi.

MABERE MARANDO AMPIGIA DEBE NGWATA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani, Mabere Marando, amewaomba wakazi wa Kata ya Mianzini kumchagua Ngwata Saulo, ili akasimamie fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Kata hiyo.

Marando alisema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mbagara Rangi tatu wialayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Alisema mtakapo mchagua Saulo mtakuwa hamkufanya kosa kwa kuwa Chadema inauhakika kuwa anao uwezo wa kuchambua bajeti na kutambua ni kiasi gani cha fedha kimetengwa na Manispaa hiyo kwa ajili ya maendeleo ya kata hiyo.

“Hata wasisi wetu wasiasa za nchi hii, enzi hizo wakati walipokuwa wakiendesha siasa walikuwa na lengo la kumng’oa mkoloni Mwiingereza hawakuwa wakipunzika kufanya siasa”alisema Marando.

Alisema Chadema ni chama makini cha upinzani chenye malengo ya kushika dola kwa kuking’oa chama tawala madarakani, ndio maana hakipunziki kufanya kazi kwa ajili ya kuwakomboa wanyonge kama Wanamianzini.

Marando alisema kutokana na malengo hayo bado yanahitaji mshikamano wenu wa dhati kwa kumchagua mgombea wa Chadema ambaye atakwenda kuwang’o mapanya wote wanaotafuna fedha zenu pale Manispaa.

Naye mgombe udiwani wa chama hicho Saulo, alisema atakapochaguliwa atahakikisha wenyeviti wa serikali za mitaa wote wa kata hiyo, wanafutwa kazi kutokana na wenyeviti hao kushiriki wenyevitendo mbalimbali vya kuwahujumu Wanamianzini.

“Mkinichagua nitamtaka mkurugenzi wa wa Manispaa hii ya Temeke aitishe uchaguzi upya ili tuweze kuchagua wenyeviti wapya ambao watafanyakazi kwa maslahi ya wanyonge bila kubagua”alisema Saulo.

Saulo alisema atahakikisha anapambana na wale wote waliojihusisha katika matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo akitolea mfano sh milioni 50 zilizotumika kujenga choo kimoja chenye matundu kumi, bila kuonyesha kimejengewa wapi.

Naye Meneja wa Kampeni hizo Jumaa Mwaipopo alisema Chama cha Mapinduzi (CCM), kimekuwaa kikishindwa katika baadhi ya chaguzi kitendo ambacho sera zake hazikubaliki tena, ni wakati sasa kwa wanamianzini kukiadhibu chama hicho kutokana na sera zake mbovu.

Uchaguzi huo mdogo unafanyika katika kata hiyo baada ya kifo cha diwani Cecilia Macha (CCM), mwaka jana, ambako uchaguzi huo utafanyika Juni 16 mwaka huu.

NSSF YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI MACHO KWA WABUNGE

$
0
0
Dk. Yasinta Shobola akimchukuwa vipimo, Mbunge wa Mfindi Kusini(CCM), Mendrad Kigola wakati wa zoezi la kupima  afya kwa wabunge lililoendeshwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Viwanja vya ukumbi wa Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Said Bungala (kulia) akipima macho wakati wa zoezi la kupima  afya kwa wabunge lililoendeshwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Viwanja vya ukumbi wa Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa Mufindi Kusini (CCM), Mendrad Kigola akipima macho wakati wa zoezi la kupima  afya kwa wabunge lililoendeshwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Viwanja vya ukumbi wa Bungeni Mjini Dodoma.

JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LATOA UFAFANUZI

$
0
0

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA


03  Juni, 2013

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepata ujumbe  kupitia simu za mkononi ambao umesambazwa kwa wananchi mbalimbali ukisadikishwa kuwa unatolewa na JWTZ. Ujumbe huo wa simu ya mkononi unasema ‘Habari zilizotufikia hivi punde. Mtanzania yeyote, kaa makini usiokote kitu chochote ambacho una shaka nacho, kunabomu zimerushwa toka nchi jirani Malawi zaidi ya 30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo kitu kipo kama chupa la chai chenye rangi ya fedha. Usiguse’
 Piga namba 0756 000042. SMS hii tuma kwa watu uwezavyo. Imetolewa na JWTZ’.

JWTZ linapenda kuwaondoa wananchi hofu kutokana na taarifa hiyo. Kwanza, Ujumbe huo haujatolewa na JWTZ. JWTZ  haliwezi likatumia mfumo huo wa SMS kuwapa wananchi wake taarifa za hatari kama hizo. Aidha, JWTZ hutangaza kupitia vyombo rasmi kama vile Magazeti, Radio na Television.
Pili, bomu la tani 100 ni zito mno,  halijawahi kutengenezwa duniani. Na kama lipo, haifahamiki bomu hilo litarushwa vipi , kwa kutumia ndege au


Mzinga?.  Lakini pia, mzinga wa aina hiyo haupo duniani kote na wala hakuna ndege yenye uwezo huo, hasa kwa bomu lenye umbile dogo kama hilo(Chupa ya Chai).
Tatu, habari hizi hazina ukweli kisayansi wala kiuhalisia au fikra za kawaida. Tunawaomba wananchi wazipuuzie taarifa hizi kwani sio za kweli ni uongo mtupu. JWTZ lipo kwa ajili ya Wanachi hivyo, kwa taarifa hizi za hatari,lazima lingewajulisha wananchi kwa njia zilizoelezwa hapo juu na si kwa simu za mkononi.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk




Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>