Na Kenneth Ngelesi, Mbarali
ZAIDI wa wanakijiji 800 kutoka kitingoji cha Magwalisi kijiji cha Nyeregete Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, wameya kimbia makazi yao baada ya kuvaniwa na wenzao wa kutoka vitongoji sita vya kijiji hicho wakiwa na mikuki,mpanga na silaa zingine za jadi kwa lengo la kuyanyang’anya mashamba yao ili wagawane.
Wanakijiji hao wamefikia hataua hiyo baada ya watu hao ambao sehemu kubwa walikuwa ni vijana kutoka vitongoji hivyo vya kijiji cha Nyeregete walisadiwa na jeshi la Polisi kutoka kituo cha Rujewa ambao walifika katika Mtaa huo na kuanza kuvunja milango ya vyumba kadhaa ambapo nyumbani 5 zilichomwa na kuteketea kwa moto.
Tukio hilo limetokea Novemba 26 mwaka huu majira ya 10:00 jioni mawaka huu, na kwamba Mkuu wa wilaya hiyo Gulamhussein Kifu ndiye anaye daiwa kuwa kinara wa mpango huo wa kupora mashamba akishikiana baadhi ya wafanyabiashara Mazar Juma kutoka katika mji wa Rujewa na Mwandulami kutoka Mkoani Njombe ambao wanafadhili mgogoro huo.
Akisimulia Mkasa huo kwa waandishi wa habari waliofika katika eneo la tukio, mwanakijiji ambaye ni muhanga wa tukio hilo aitwaye Mkima Luhende kutoka kitongoji hicho alisema kuwa siku ya tukio Polisi kwa kushikiana na vijana 80 kutoka katika vitongoji sita ambavyo ni Lyahamile,Tembo A na B,Simba,Nyati,Nyaluanga, walifika kwenya mashamba yao na kuanza kupima kwa lengo la kuayagawa kwa kila aliye kuepo katika eneo hilo.
Baada ya kuanza kwa zoezi hilo Luhende alisema kuwa waliamua kusimama kila mmoja katika shamba lake kwa lengo la kuzuia zoezi hilo lisiendelee na ndipo walipoanza kushushiwa kipigo na wavamizi hao waliyo kuwa wakisadiwa ba jeshi la polisi ambao walikuwa wakipiga mabomu kwa lengo la kuwa ogofya wakulima.
Akizungumza kwa uchungu Luhende alisema kuwa baada ya kushushiwa kipigo hicho, waliamua kukimbia makazi yao na ndipo polisi kwa kushirikiana na vijana wa Nyeregete walipoanza kuvamia makazi yao na kupora vita mbalimbali zikewemo fedha taslimu sh mil 2 .
Luhende aliongeza kuwa mbali na kuchukua kiasi hicho cha fedha, wavamizi hao pia walipora, betri tatu za gari,magania,10 ya mpunga,kuku 20, simu zisiozo na idadai ambazo zilikuwa zinachajiwa,seti ya makochi pamoja na mito yake.
Hata hivyo Luhende ambaye ni mmoja watu ambao mashamba yana windwa na wahusika hao ambaye anamiliki ekari 20, alisema ni muendelezo wa kuwa nyanyasa watu wa jamii ya kisukuma wanaoishi katika Wilaya ya Mbarali na kumiliki ardhi kwani kitongoji hicho ndicho pekee kina kaliwa na watu wa jamii hiyo.
Mkulima mwingine aliye patwa na mkasa wa kuporwa mali ni Nkuba Mahalu alisema kuwa wavamiwa hao walifika nyumbani kwake na kupora gunia kumi za mpunga na seti moja ya kochi, kabla ya kuhamia kwenye nyumba ya mwanamke aitwaye Johari Mohamed ambaye walifanyia vurugu kabla kabla kuchukua begi lake la nguo ambalo ndani yake kulikuwa na sh 800,000/ na kubomoa vienge vya mahindi na kisha kumwagia maji.
Mbali huyo mwanamke mwingine katika kitongoji hicho Kwangu Deus anadiwa kupotelewa na watoto sita ambao walikimbia baada ya uvamizi kufuatia kelele za mabomu, na kwamba mpaka waandiashi wanaondoka eneo na tukio Novemba 28 majira ya saa 12:jioni mwaka huu walikuwa hawajulikana walipo akiwemo mumewe na watoto wengine wa mjirani.
Hata hivyo baadhi ya wanakijiji walio zungumza na waandishi wa habari walidai kuwa mpango huo wa kuporwa ardhi, unaratibwa na Mkuu wa wilaya hiyo Kifu kwa kuwatumia vijana hao ili waipole ardhi ili baadaye wagawe kwa wafanyabiashara hao.
“Ndugu zangu wana habari ni vema mkafamu kuwa mpango huu wa kupora ardhi yetu unaratibiwa na mkuu wetu wa wilaya, akishirikiana baadhi ya watendaji kutoka mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa kwani sisi ndo watu wa kwanza kutoa taarifa kwake lajkini hakuna hatua zozote alizo chukua”,alisikika mwananchi mmoja
Walisema kuwa kitu kingine kinacho fanya waamini kuwa mpango huo upo chini ya Mkuu huyo wa wilaya ni kwamba mbali kufanyiwa uvamizi huo lakini bado jeshi la polisi kituo cha Rujewa kina washikiria wananchi 12 na watoto 4 chini ya miaka 14 kutoka katika kitongoji hicho ambao kimsingi ndiyo waliyo fanyiwa fujo.
Walisema kuwa katika hatua niyingine vitu walivyo kuwa wakiporwa vilikuwa vinasombwa kwa kutmia magari ya Polisi yaliyo kuwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kuwasomba wanachi hao ambao hata hivyo wengi wao wamekimbia makazio yao kwa zaidi ya siku tatu kwa kugopwa kukamatwa na polisi nanyo ni kuku,mahaindi na magodoro,.
Wogo wawa wanchi hao ulidhirishwa wakati gari la waandishi likiwasili katika kitiongoji wengi wao walianza kukimbia lakini juhudi za wenzao wal;ianza kuwa p9gioa siomu wakiwa taka kurejea katika makazi yao kwani gari lilikuwa limewabeba waandishi wa habari na si maadui zao.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SSP Diwani Athuman akizungumzia suala hilo alithibitisha kuwa na taarifa za tukio hilo,na kwamba jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi.
Aidha Diwani aliongeza kuwa katika tukio hilo ni kwamba taarifa alizopewa na OCD wa Mbarali zinasema kuwa mpaka jana jioni watu kumi ndiyo walikuwa wanashirikiliwa na jeshi polisi kituo cha Rujewa.
Kamanda huyo wa Polisi alikiri kuwa mgogoro huo unachochewa na Mkuu huyo wa wilaya na kwamba wananchi wa kitongoji cha Magwalisi wanaonewa kwani ardhi hiyo wana miliki kiharari kuanzia mwaka 1973 walipo hamia katika eneo hilo.
Hata hivyo mara baada ya kutoka eneo la tukio waandishi wa habari walitamtafuta Mkuu huyo wa wilaya kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi juu ya suala hilo,lakini simu yeke iliita bila kupokelewa, na baadaye kutopatikana baada ya kuzimwa.