Wateja wa Skylight Band wiki iliyopita walipata nafasi ya kuburudika na kinywaji kipya kabisa toka nchini Sweden MOKAI Cult ambacho kina Alcohol 4.5 yenye ladha murua kama aina ya Savanna ambacho ni zaidi ya Savanna.
Hakika wateja wa Skylight Band katika ukumbi wa Thai village Masaki wiki iliyopita walichangamka kweli na kinywaji hiki toka huko Sweden chenye Alchohol ya wastani ambayo mtu anaweza kumudu kunywa na kuamka safi kabisa bila Hang-Over.
Mashabiki wa Skylight Band wakiingia getini walipata fursa ya kuonjeshwa kinywaji hicho kipya kutoka Sweden kinachotambulika kama MOKAI Cult ambacho kitakuwepo kila siku ya Ijumaa ndani ya Thai Village jijini Dar na kuzidi kuwachangamsha mashabiki wa Bendi hiyo kusakata Rhumba zaidi.
Mrembo wa MOKAI Cult akifafanua jambo kwa wateja juu ya kinywaji hicho kipya.
Mbunifu wa Mavazi Gabriel Mollel akiuza sura na Models Neema Mbuya pamoja na Anna.
Miss Tanzania 2011 Salha Israel (wa tatu kulia) kwenye picha ya pamoja na marafiki zake ndani ya Thai Village-Masaki jijini Dar Juma lililopita.
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakipata Ukodak na Warembo wa MOKAI Cult waliokuwa wakaribu kwa wateja na kutoa huduma yenye kiwango cha kimataifa. Njoo wewe na yule leo tujikoki na MOKAI.
Rappa wa Skylight Band Joniko Flower akiongoza makamuzi na kikosi kazi cha band hiyo kutoa burudani kwa mashabiki wake Ijumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa Thai Village jijini Dar.
Divas wa Skylight Band wakiongozwa na Aneth Kushaba AK47 katika burudani ya aina yake yenye kiwango cha kimataifa kwa mashabiki wake.
Digna Mbepera akikamua jukwaani huku akipewa Back-Up na Mary Lucos pamoja na Winfrida.
Wo! I feel good, I knew that I wouldn't of.....I feel good, I knew that I wouldn't of.....So good, so good, I got you......Joniko Flower, Aneth Kushaba sambamba na Irene binti mwenye kipaji cha kutumia "Saxophone" .
Irene akipuliza Saxophone.
Mchaka mchaka mwanzo mwisho hapa chezea Skylight Band.
Mzuka ukiwa umempanda Sam Mapenzi wa Skylight Band.
Mdau Alois Ngonyani kama kawaida yake hakubali kushindwa.....!
Warembo wa MOKAI na miondoko ya "Yachuma Chuma".
Joniko Flower akitangaza zawadi kwa mtu atakayecheza vizuri atajishindia chupa mbili za MOKAI.
Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band akijimwaga jukwaani kuonyesha umahiri wake.
Na mwishowe alikabidhiwa zawadi ya chupa mbili za MOKAI pamoja na kupata Ukodak na warembo wa kinywaji cha MOKAI Cult.
Zawadi ziliendelea kugawiwa kama inavyoonekana pichani.
Bado nimo kumbeeee.....!...Wababa nao hawakubaki nyuma kwenye burudani.
Wadau wetu wa ukweli wakipata Ukodak.
Dk. Sebastian Ndege akishow love na mmoja wa marafiki zake kutoka Mwanza.
Hapo vipi?? Bata mwanzo mwisho na MOKAI halali mtu hapa mpaka kieleweke.
Familia ya Skylight Band.
Wadau wakifurahia Ukodak.
Shika Moyo.......x3........Warembo wa MOKAI wakicheza sebene la Skylight Band.