Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 5

$
0
0
VEE MONEY AISAMBAZA 'COME OVER'
Na Elizabeth John



MWANADADA ambaye anakuja juu katika tasnia ya muziki wa bongo fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesambaza kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Come Over’ hivi karibuni.

Kabla ya kutaka kusambaza ngoma hiyo, Vanesa alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Closer’ ambacho kinafanya vizuri, pamoja na kushirikiana vema na mkali wa bongo fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ katika kibao chao cha ‘Me and You’.

Kwa mujibu wa Vanessa, anaomba mashabiki wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hii ambayo anaimani itafanya vizuri kutokana na mashairi yaliyopo ndani yake.

“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hiyo ambayo ipo jikoni naimani nitaanza kuisambaza mwisho wa mwezi huu,” alisema.

Alisema huo ni ujio wake mpya ni tofauti mashabiki walivyozoea kumuana katika nyimbo ya ‘Bashasha’ aliyoimba na Bob Junior pamoja na wimbo wake wa ‘Monifere’, na kwamba kazi hiyo imetengenezwa na mmoja wa kundi la Navy Kenzo, Nahreel.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>