Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Bi. Samia Suluhu afunika mkutano wa kampeni Kibaha

$
0
0
WanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, ambapo mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) alihutubia.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.
Mmoja wa wasanii wa kugani mashairi akiwaburudisha wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, ambapo mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) alihutubia.

Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa ya CCM, Anjela Kairuki, akizungumza kumnadi mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) kwenye mkutano wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe.

Kikundi cha akinamama wajasiliamali na utamaduni kutoka Temeke kikitoa burudani kwa umati na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais,  katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe.

Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (kulia) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani, Subira Mgalu katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.

Aliyekuwa mbunge wa Nkenge na mjumbe wa kamati ya kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Bi. Asumpta Mshama (katikati) akiwagawia zawadi ya kanga wanakikundi cha akinamama wajasiriamai cha Temeke katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu (kulia) akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Said Jafo (kushoto) katikati ni mgombea udiwani, Mwishehe Mlao mkoani Pwani, 

Baadhi ya wagombea nafasi za udiwani CCM Jimbo la Kisarawe, mkoani Pwani wakitambulishwa katika mkutano wa kampeni. 

Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (kushoto) akipewa zawadi na baadhi ya akinamama mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.

Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (kushoto) akipewa zawadi na baadhi ya akinamama mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.
Msanii Snura (katikati) akitoa burudani kwa Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni leo.
Wema Sepetu akizungumza na Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni leo.

Chipukizi wa CCM wakitoa burudani katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Koka Francis (kulia) akizungumza jambo na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais Bi. Samia Suluhu. 

Mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi ya CHADEMA toka kwa Katibu wa Hamasa Taifa wa CHADEMA, Bwana Nyakarungu (kulia) mara baada ya kujiunga CCM leo.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Koka Francis akimvalisha sare za CCM Katibu wa Hamasa Taifa wa CHADEMA, Bwana Nyakarungu mara baada ya kujiunga CCM leo.
Picha zote/www.thehabari.com


Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>