Mkurugenzi Mtendaji wa GGM Mr. Terry Mulpeter (Kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Shs 300 Million kwa uongozi wa timu ya Geita Gold Sports Club ya Geita. Katikati ni Mwenyekiti Msaidizi wa timu hiyo Ally Twist na kulia ni Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa bwana Deodatus Kayangu.
Na Mwandishi Wetu
Akizungumza wakati wa kukabidhi check hiyo, Meneja wa Mgodi wa Geita MR. Terry Mulpeter, alisema “ GGM inajivunia kushiriki katika ufadhili wa timu hii ya hapa Geita, Ufadhili huu ni zaidi ya fedha tunazotoa, ni uboreshaji wa mahusiano katika jamii yetu na uhamasishaji wa mazoezi kwa ajili ya afya bora za wanajamii wanaozunguka mgodi wa Geita”
Timu ya Geita Gold, inashiriki daraja la kwanza na imesajili wachezaji 30 katika msimu huu wa ligi kuu. Uongozi wa timu ulishukuru kwa ufadhili wa fedha hizo ambazo zitatumika katika utoaji wa posho, usafirishaji wa wachezaji na malazi wakati wakiwa kwenye ligi.
Mwenyekiti msaidizi wa timu hiyo bwana Ally Twisti alisema “ Ufadhili wa GGM kwenye timu yetu utatupa boost ya ushiriki kwenye ligi hii, tunatambua kwamba GGM imekuwa ikifadhili timu yetu huko nyuma lakini kwa ufadhili wa mwaka huu tunatarajia kushinda kombe hapo mwakani”
GGM imejikita katika kufadhili shughuli zinazoleta chahu ya maendeleo katika jamii ikiwa ni pamoja na michezo. Mgodi unatambua kwamba michezo ni kiunganishi muhimu katika kujenga mahusiano katika jamii zote duniani na pia huleta afya na utunzaji wa tamaduni ambazo zinahamasisha jamii kuwa na taifa bora lenye watu watakaoshiriki vyema katika uchapakazi na kuleta maendeleo halisi kwenye jamii.
Timu ya Geita Gold sports Club ya mjini Geita ikipiga picha ya baada ya kusaini mkataba wa ufadhili wa timu hiyo na kukabidhiwa hundi ya Tshs 300 Million kwa msimu wa 2015/16 ligi ya daraja la kwanza.