Na Ashura Jumapili, Bukoba,
MWANAFUNZI wa kidato cha tano Ezra Gerald Wambamba (19 )wa kombi ya CBG katika shule ya sekondari ya wavulana Ihungo iliyoko Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, amejinyonga kwa kutumia shuka hadi kufa kwa madai ya kukosa huduma ya matibabu akiwa hospitali.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Gilles Muroto, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 16 mwaka huu majira ya saa moja, asubuhi katika hospitali ya Mkoa wa Kagera, alikokuwa amelazwa mwanafunzi huyo anayetoka maeneo ya Kitete mkoani Tabora.
Muroto,alisema, mwanafunzi huyo alijinyonga kwaku tumia shuka hadi kufa umbali wa mita 73 kutoka wodi namba tatu alikokuwa,amelazwa mwanafunzi huyo alifunga shuka hiyo juu ya mti na kujinyonga.
Alisema,alilazwa hospitali hapo tangu Septemba 11 mwaka huu na kugundulika kuwa anasumbuliwa na homa ya typhoid hadi 16 alipoamua kujinyonga.
Alisema,mwili wa marehemu, ulipopekuliwa na jeshi la polisi alikutwa na kipandae cha karatasi kilichoandikwa ujumbe unaosemeka hivi ”haiwezekani binadamu kuhudumiwa kama mbwa yaani nafika hospitali najieleza hali yangu halafu daktari ananiandikia kulazwa bila kupimwa,sasa sijui natibiwa nini?kwakweli siwezi kuvumilia yaani wenzangu wanasoma halafu mimi nimekalishwa tu hapa hosipital bila ya kujua natibiwa nini?,inaniuma sana mpaka kufikia hatua hii kujiondoa duniani kwa sababu ninaona watu
wanachezea ndoto zangu mimi siwezi kuona ndoto yangu inazimwa wakati inatakiwa niwepo shuleni nikamilishe ndoto zangu.”
Alisemabaada yakuandikaujumbehuoakamaliziakwakusema “mjitahidi tukutane mbinguni”mwishoakaandikanenolakiingereza( respect myfamily and Henry).
Aliongeza kuwa katika tukio hilo hakuna ,aliyekamatwa uchunguzi unaendelea kuhusiana na kifo hicho cha mwanafunzi.
Kwa upande wake katibu wa hospitali ya mkoa wa Kagera Benges Justus alithibitisha kutokea kwa tukio la mwanafunzi kujinyonga hadi kufa septemba 16 mwaka huu majira ya saa moja na nusu asubuhi.
Benges,alisema mwanafunzi huyo alipokelewa hospitalini hapo septemba 15na baada yakufanyiwa uchunguzi wa kitabibu wa vipimo vyote ilibainika kuwa anasumbuliwa na maralia hivyo kuanzishiwa tibaya maralia.
Alipohojiwa kamamgonjwa huyo alikuwa na typhoid alisema vipimo vilionyesha maralia na siyo typhoid.
Hata hivyo alisema uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi huyo unaendelea ilikubaini kilichomuua. Chanzo cha habari Tanzania Daima.