Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659
↧

TOUCHROAD-MR UK INTERNATIONAL MARATHON 2024 YAJA KIVINGINE

$
0
0

Makamu Mwenyekiti Riadha Dar es Salaam (DAA), Peter Palangyo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 

NA TULLO CHAMBO, RT

MSIMU wa tatu wa mbio za kimataifa za Touchroad Mr. UK Marathon zinazotarajiwa kurindima September 24 jijini Dar es Salaam umezinduliwa rasmi huku mwaka huu zikija na maudhui mapya kabisa 'Kimbia Kukuza Utalii na Mahusiano ya Kimataifa'.


Uzinduzi huo umefanyika kwenye hoteli ya Peacock September 15 na kuhudhuriwa na waandaaji, wadhamini na waandishi wa habari.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Mratibu wa mbio hizo, Nelson Mrashani, alisema Mr. UK International Marathon ni ya viwango vya kimataifa katika suala la ufundi na ushiriki wa wakimbiaji kutoka nje ya nchi.


Mrashani, alisema mwaka humu mbio hizo zitafanyika September 24 kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.


"MR UK Sports pamoja na Touchroad Holdings Company Group, wamepanga kwa mafanikio makubwa MR UK Marathon kwa miaka miwili mfululizo jijini Dar es Salaam, kijamii, kiuchumu na kiafya kwa wale waliishiriki ndani yake. Tumerudisha pia kwa jamii pana kwa njia mbalimbali kama kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo hospitali ya MOI na vifaa vya uzazi hospitali ya Wilaya Kinondoni," alisema Mrashani na kuongeza.


Mwaka huu tutakuwa na maudhui mapya kabisa, kauli mbiu tutakayokimbia nayo ni 'Kimbia Kukuza Utalii na Mahusiano ya Kimataifa'.


"Kwa kutimiza azma hii, tumeshirikiana kwa mafanikio na kampuni ya Touchroad International Holdings Group kutoka China, kuandaa mbio hizi na kuunganisha urafiki kati ya China na Tanzania na nchi jirani kupitia utalii wa michezo," alibainisha Mrashani.


Mratibu huyo, aliongeza kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii ambavyo hata baadhi ya wenyeji hawajatembelea bado, hivyo kupitia tukio hilo watahakikisha kuwa watu wanatambua utofauti wa vivutio vilivyopo nchini.


Alisema wanatarajia washiriki zaidi ya 100 kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kukimbia na kufanya utalii nchini, huku lengo la jumla ni kuwa na washiriki zaidi ya 5000 mwaka huu.


Mrashani akizungumzia upande wa zawadi, alisema mwaka huu wameboresha na watazawadiwa mshindi wa kwanza hadi wa 15, lakini pia kukiwa na zawadi kwa watu wazima, wazee na watoto.


Alisema mbio hizo ambazo ni Km. 21, Km. 10 na Km. 5 za kujifurahisha huku usajili rasmi umefunguliwa kupitia mtandao www.mrukmarathon.co.tz na utaweza kulipia kupitia Tigo Lipa namba 6687999 na Vodacom 5001515 na mshiriki anapaswa kutunza ujumbe wa malipo kwa ajili ya wakati wa kuchukua vifaa vya kukimbilia.


Waandaaji hao walishukuru ushirikiano wanaopata kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wizara yenye dhamana na michezo, Jeshi la Polisi na wadhamini mbalimbali ikiwemo MR UK Electronics, SGA, Bonite Bottlers, Zara Tours, Peacock Hotel na wengineo na kwamba wadhamini na wadau wengine zaidi wanakaribishwa.

↧

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Latest Images

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>