Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Mbeya city wasema ufadhili Binsulum haukidhi mahitaji ya timu

$
0
0

Na Keneth Ngelesi, Mbeya

UONGOZi wa timu ya soka ya Mbeya City inayoshiriliki ligi kuu Tanzania bara ya kutoka Mbeya  umesema kuwa licha ya kuingia mtakaba wa Binsulumu kudhamini timu hiyo lakini bado inahitaji mchango wa kila hali kutokana na kiwango hicho kuto kidhi mahitaji yote ya timu hiyo.

Akizungumza na wachama wa timu hiyo tawi la Sido katika hafla ya kuipongeza timu hiyo kwa kufanya vizuri katika msimu uliopita na kuukaribisha  msimu mpya iliyo andaliwa na tawi hilo na kilifanyika katika Hotel Gr jiji hapa katibu huyo alisema fedha hizo kitapunguza ukali wa mahitaji.

Hata hivyo Katibu alifikia hatua ya kutoa hilo baada ya mashabiki hao kuhoji uongozi huo kwamba mara ya kwanza mashabiki walikuwa wanajisafirisha kwa fedha zao kwenda na timu hiyo sasa uongozi huo hauoni haja ya kuchangia nauli kwa mashabiki kutokana na kuanza kupata wadhamini?

 Akifafanunua zaidi Kimbe alisema kuwa uendeshaji wa ni ghama kubwa kwani kwa msimu uliopita jumla ya shilingi milioni 800 zilitumika hivyo kitendo cha kuanza kupata wadhamini kama Binsulumu ambaye wamesaini mkataba misimu miwili kwa milioni 300 wamepunguza makali lakini bado fedha zinahitaji kwa ajili ya kikosi hicho hata zile zinazotolewa na mdhamini  wa ligi hazitoshi.

Alisema kutokana na hali hiyo itakuwa vigumu kwa uongozi huo kuendelera kutenga fedha kwa ajili ya mashabiki lakini wataendelea na utaratibu wa  awali wa kutoa vifaa vya michezo zikiwemo jezi na vifaa vingine kwenye matawi ili fedha zinazo patikana kutokana uuzaji vya vifaa hivyo ziweze kusadia nauali kwa mashabiki.

Hata hivyo katika hatua nyingine katibu huyo alisema kuwa ni vema mashabiki wa timu hiyo wakashiriki kupiga vita uuzaji ya jezi feki ambazo zinasabisha timu kukosa mapato kutokana na watu kununua jezi feki na kwamba kila mdau wa soka ana wajibu wa kushiriki katika vita hiyo ili kunusuru wizi huo.

‘Kwa sasa kuna jezi nyingi ni feki  zinavaliwa na ndugu zenu na wangine wanaziuza lakini tukiwa kamata na kuwa peleka polisi mna kuja mkidau ndugu zena mkiwataka  tuwafutie kesi kama kweli huyo ni ndugu yako kwanini usaimzuie kuuza jezi feki badala ya kusubiri akamatwe ndo uanze kusema ndugu yako?’alihoji Kimbe.

‘Ndugu zangu wapenzi na mashabiki wa soka kutoka Mkoani  Mbeya ni vema mkajua wazi kuwa mnapo bariki uuzaji wa jezi  feki mitaani ndo mwanzo wa kuuza timu hivyo ni vema tukashirikiana kwa pamoja kupiga vita uuzaji huu wa jezi feki”.aliongeza Kimbe'

Mbali na hilo kimbe aliwaonya mashabiki wanao zomea timu za Mkoa wa Mbeya yahani Tanzania Prisons na Mbeya na kujiita mashabiki wa Yanga na Simba kuwa watu wamekosa uzalendo kwani hata timu hizo kubwa zinakuja mkoani hapa kuwa vilabu hivyo vipo lakini pindi zikishuka watakosa kuona michezo wa ligi kuu hivyo ni vema wakaungana  kuziunga timu za Mkoa wao.

Katika hafla hiyo  ambayo ilishikikisha pia wachezaji wa timu hiyo ambapo kila mmoja alikabidhiwa kitita cha sahilingi 50,000/ kutoka wadhamini wa sherehe kampuni ya TBL kupitia kinywaji cha Castlle lager fedha hizo zitolewa na Meneja matukio kanda ya nyanda za juu kusioni Abubakar Masohi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>