Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 1

$
0
0
WAKAZI  MTO WA MBU  NA WAFANYAKAZI  WA HIFADHI YA  ZIWA MANYARA WASHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA
 Wakazi wa kata ya Mto wa Mbu wakifanya usafi kuzunguka maeneo ya makazi yao, wakishirikiana na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara.
 Taka zikiondolewa.

Na Mahmoud Ahmad, Arusha

Baadhi ya wananchi wa kata ya mto wa mbu wakiwa na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara wakishiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye mji wa Mto wa Mbu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya uhifadhi duniani

Wakazi hao wa Kata ya Mto wa Mbu waliwapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kuacha shughuli zao kwenda kuhimiza usafi wa mazingira ya mji wao huku wakiwataka wenzao kujali usafi wa mazingira ilikuepuka magonjwa ya milipuko

Kwa upande wake Kaimu Mhifadhi wa Hifadhi ya ziwa Manyara Ibrahimu Yamola alisema kuwa wakazi hao ambao ni jirani na mbuga hiyo wnapaswa kuyajali mazingira wanamo ishi kwa kyaweka katika hali ya kuvutia kwani mji wao unapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbal;i wanaokuja kutembelea mbuga hizo

Akitanabaisha kuwa siku ya uhifadhi duniani inasherehekewa duniani kote na hapa nchini imekuwa ikisherehekewa kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujirani mwema kama tulivyofanya leo kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kata ya mto wa mbu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>