Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 1

$
0
0
CCM waanza mkakati wa kumng’oa  Sugu


NA KENNETH NGELESI, MBEYA

BARAZA la umoja  wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (Uvccm), Mkoa wa Mbeya, leo (Julai 5)wanatarajia kufanya mkutano wa mwaka, sanjari na shughuli ya kuapishwa kwa makamanda 11 wa umoja huo  katika ngazi ya Mkoa na Wilaya.

Umoja huo umebadilisha utaratibu  wa awali wa kuwa kuwasimika badala yake watakuwa wakila kiapo ambapo kwa mkoa wa Mbeya ndo umeanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  katika ofisini za umoja huo, Mwenyekiti wa Uv-ccm mkoa, Aman Kajuna,  alisema mkutano huo wa mwaka wa kikanuni utakuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo kujadili changamoto ndani ya chama.

Kajuna alisema kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa, Jijini hapa, atakuwa ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na ushirika, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.

Alisema miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ndani ya mkutano huo ni kuweka  mikakjati na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu.

“Kwa kweli licha ya kuwa na  mikakati ya uchaguzi wa serikali za mitaa, pia tutajadili changamoto za uchaguzi Mkuu ujao, ikiwemo mikakati ya kurejesha jimbo la Mbeya mjini tulilowaazima hawa wenzetu” alisema Kajuna.

Akifafanua zaidi Kajuna alisema  CCM inauhakika wa kulikomboa jimbo hilo kutokana na ukweli kuwa mbunge aliyepo ameonekana kupwaya.

Jimbo la Mbeya mjini linaongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia  mbunge wake, Joseph Mbilinyi  , aliyemshinda mgombea wa CCM, Benson Mpesya, ambaye ambaye alibwagwa katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kwa upande wake katibu wa Umoja huo, Said Yasin, alisema baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa baraza, siku itakayofuata  ya Julai 6 kutakuwa na shughuli ya kusimikwa kwa makamanda 11 wa umoja huo katika ngazi ya mkoa na Wilaya.

Alisema atakayefanya shughuli ya kuwasimika makamanda hao ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Taifa , Jerry Silaa, itakayofanyika katika viwanmja vya Ruanda Nzovwe.

Aliwataja makada wa chama hicho watakaosimikwa  kuwa ni kamanda wa umoja huo ngazi ya Mkoa kuwa ni Yona Sonelo, anayefanya shughuli zake Jijini Dar es salaam.

Mak amanda wengine na  Wilaya zao kwenye mabano kuwa ni Philipo Mulugo (Chunya), Tonebu Chaula (Mbeya Mjini), Oran Njeza (Mbeya Vijijini).

wengine watakao apishwa Ibrahmu Mwakabwanga (Mbarali), Ibrahm Mwanjilinji (Mbozi), Richard Kasesela (Rungwe), Elius Asangalwisye (Kyela), Twaha Kalabeba (Momba) na Gidion Cheyo (Ileje).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>