Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
JESHI la Polisi Mkoani hapa limefanikiwa kumuua jambazi Joseph Kapinga Mkazi wa Mafiga Mkoani Morogoro akiwa na silaha aina ya Ak 47 yenye risasi 25 kwenye magazine.
Tukio hilo limetokea June 19 mwaka huu majira ya saa 11 alfajili ambapo askari polisi waliwakuta na watu hao baada kupokea taarifa kotuka kwa walinzi wa soko kuu Tunduma baada ya kuwatilia shaka watu hao ambao walikuwa wawili kutokana na mavazi walio vaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jiji hapa Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa hizo askari waliokuwa doria walianza msako mkali wa kuwatafuta watu hao ambapo waliwakuta eneo la Msikiti wa Tunduma.
Kamanda msangi alisema kuwa kutokana msako huo walifanikiwa kuwaona watu hao wawili wakiwa wamevalia makoti makubwa meusi huku mwingine akiwa amebeba mfuko mkubwa ambao unaadiwa ulikuwa silaha.
Alisema kuwa Kamanda mara baada ya kuwaona watu hao waliwasimamisha na kuwa amuru wa simame hata hivyo baada ya majambazi hao kubaini kuwa waliokuwa wakiwa simamisha ni askari walianza kukimbia na mmoja kati yao aliyekuwa amevaa jaketi jeusi alikimbia kwa umbali wa mita ishirini na kuanza kufyatua risasi hovyo huku akielekea eneo waliko askari.
Alisema baada ya kuona kuona hali hiyo polisi walijibu mapigo na katika majibizano hayo ya kurushiana risasi jambazi Kapinga ambaye alikuwa akitumia bunduki aina AK.47 yenye namba 592058 na iliyo kuwa na risasi 25 kwenye alikufa papo hapo.
Kamanda Msangi alisema mara baada polisi kufanikiwa kupigfa risasi jambazi walikuta na kitambulisha cha mpiga kura mbacho kinaonyasha alijinadikisha Songea Mkoani Ruvuma huku Makazi wa yake yakiwa Mafiga Morogoro.
Aidha msangi aliongeza kuwa kuwa katika tukio hilo hakuna madhara kwa wananchi wala askari aliye dhurika katika purukushani hizo na kwamba jeshi linaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuendelea kumsaka jambazi aliye kimbia jambazi mwingine.