Warembo wanaowania taji la Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa katika pozi.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa atakuwa mgeni rasmi katika shindano la kumsaka mrembo wa mkoa huo, Nice & Lovely Miss Tanga 2014, shindano ambalo litafanyika mwishoni mwa wiki hii jumamosi ya tarehe 21 June 2014 Mkonge Hotel.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mac D Promotions ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Irene Rweyunga amesema kuwa, Mkuu wa mkoa wa Tanga mbali na kuwa mgeni rasmi siku hiyo, amepongeza maandalizi makubwa ya kuridhisha yaliyofanyika mpaka sasa kabla ya kufanyika kwa shindano hilo.
"Nafurahi kusema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia mia moja, na washiriki wote 14 wapo kambini wiki ya pili sasa katika hoteli ya Tanga Beach Resort chini ya mwalimu wao Mariam Bandawe, alisema Irene.
Warembo wanaowania taji la Nice & Lovely Miss Tanga 2014 ni Zuhura Masoud, Irene Hermes, Diana Festo, Fatma Iddy, Faith Joel, Elvira Arbogast, Abigael Mathias na Yusta Philip. Washiriki wengine ni Nasra Ramadhan, Upendo Lyimo, Degy Wilfred, Pendo Ayoub na Janeth Maimu
Irene amesema mshindi wa kwanza atazawadiwa gari dogo la kifahari aina ya Toyota Vitz, gari ambalo lipo mkoani Tanga wiki ya tatu sasa, na washindi wengine watazawadia fedha taslimu usiku huo.
Mshindi wa pili atapewa shilingi laki tano, mshindi wa tatu atapewa shilingi laki mbili na nusu, mshindi wa nne atapewa shilingi laki moja.
Washiriki wengine wote waliosalia watapewa shilingi elfu hamsini kila mmoja. Katika shindano hilo ambalo limedhaminiwa na Nice & Lovely, EATV, Redd's, Tanga Beach Resort, Breeze Fm, CXC Afrca, Rweyunga Blog na Mwambao Fm, burudani itatolewa na Malikia wa mipasho wa Afrika Mashariki na Kati, Hadija Omary Kopa.