Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 0

$
0
0
UZINDUZI WA KAMPUNI MPYA YA VIFAA VYA UJENZI STONE BLOCK COMPANY WALETA TIJA KATIKA SEKTA YA UJENZI NCHINI
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Hussein Mwinyi pamoja na Waziri wa Biashara na Forodha kutoka Uturuki Mh. Hayati Yazici wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kampuni ya vifaa vya ujenzi Stone Block Building  uliofanyika katika kampuni hiyo iliyopo Kawe Darajani jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wakafanyakazi wa Kampuni ya Stone Block Building wakishuhudia uzinduzi huo.
 Mfano wa choo kilichotengenezwa na vifaa vinavyotengenezwa na Kampuni ya Stone Block Building.
  Mfano wa choo kilichotengenezwa na vifaa vinavyotengenezwa na Kampuni ya Stone Block Building.
 Mfano wa choo kilichotengenezwa na vifaa vinavyotengenezwa na Kampuni ya Stone Block Building.
 Baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Stone Block Building,
Baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Stone Block Building,
 Vifaa vinavyotengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Stone Block Building,
 Baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Stone Block Building,
Baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Stone Block Building,
Baadha ya vifaa vya ujenzi.
Vijana wa kituo cha Kigamboni wakitoa burudani katika uzinduzi wa Kampuni ya vifaa vya ujenzi Stone Block Building  uliofanyika jana katika kampuni hiyo iliyopo Kawe Darajani jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM, Tanzania

Mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda yalifanyika jana baada ya kuzinduliwa kampuni ya Stone Block Company ambayo itakuwa ikizalisha vifaa mbalilmbali vya ujenzi hapa nchini. 

Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Taifa Mh. Husein Mwinyi, pamoja na Balozi wa Uturuki nchini Balozi Ali Davutoglu, Waziri wa Biashara na Forodha kutoka Uturuki Mh. Hayati Yazici, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wabunge mbalimbali kutoka Uturuki.

Uzinduzi huo ni kufuatia uhitaji mkubwa wa vifaa vya ujenzi  nchini  suala ambalo linaleta msukumo na kuwafanya wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki kuamua kuwekeza nchini ili kuhakikisha watanzania wanapata vifaa vya ujenzi kirahisi na kwa gharama nafuu kwani itapunguza gharama za usafirishaji wa vifaa hivyo kutoka nchi za nje.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Waziri wa  Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Husein Mwinyi aliwashukuru sana wawekezaji hao kwa kulea mapindunzi katika sekta ya ujenzi na pia amewataka watanzania kuchangamkia fursa  kwani hii itawapa mwanya wa  ajira na biashara kwa ujumla. 

“Hii ni fursa kwa watanzania wote, kampuni hii itazalisha vifaa vya ujenzi hapahapa nchini na hii inathibitisha mapinduzi makubwa katika sekta ya ujenzi na ya biashara pia. Hii ni kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi yetu na nchi ya Uturuki kwani tumekuwa tukifanya mahusiano makubwa ya biashara suala linalotufanya kufaidika kwa fursa mbalimbali”.

Nae Waziri wa Biashara na Forodha kutoka nchini Uturuki Mh. Hayati Yazici amewashukuru watanzania kwa kuipokea kampuni hiyo ya ‘Stone Block Building’ kwani hii inazidi kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya nchi hizi mbili.

 “Ujenzi ni sekta muhimu isiyoisha mahitaji, pia teknolojia inabadilisha mahitaji, hivyo ujenzi wa kisasa unahitaji vifaa vya kisasa zaidi. Tanzania itanufaika na vifaa vya kisasa kutoka katika kampuni hii mpya. Tunaamini tutashirikiana na watanzania katika kuleta maendeleo katika sekta hii ya ujenzi”alieleza Mh. Yazici.

 Tanzania imekuwa na mahusiano ya muda mrefu na nchi ya Uturuki katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na elimu suala linalopelekea watanzania kunufaika zaidi. 

Hafla hiyo iliudhuriwa na watanzania mbalimbali huku wakiwa na shauku ya kuchangamkia fursa katika kampuni hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>