Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 3

$
0
0
NSSF YATOA ELIMU KUHUSU HIFADHI YA JAMII KWA WANACHUO WA CBE
 Mkurugenzi wa Wanafunzi wanaochukua Mafunzo ya Shahada ya kwanza katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dk. Esther Mbise akimkaribisha mgeni rasmi, Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii ( NSSF), Eunice Chiume (katikati),wakati wa Semina kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), iliyofanyika katika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko chuoni hapo, Felix Chale. Jumla ya wanachuo 180 walihudhuria semina hiyo.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akitoa mada wakati wa semina ya kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu kuwa na uelewa kuhusu Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF), pindi watakapomaliza elimu yao.
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini, Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati akitoa mada katika semina hiyo.
 Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akitoa mada kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NSSF.
Tunasikiliza kwa makini.
 Baadhi ya maofisa wa NSSF wakigawa vipeperushi vyenye maelezo ya muhimu kuhusu NSSF.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akigawa vipeperushi kwa wanafunzi wa CBE wakati wa semina hiyo.
 Tunajifunza hifadhi ya jamii.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha CBE wakisikiliza kwa makini kazi za mfuko wa hifadhi ya jamii na faida zake
 Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akijibu maswali ya wanafunzi wa CBE kuhusiana na mfuko wa Taifa Hifadhi ya Jamii wa NSSF.
 Jonas Pera akiuliza swali.
 Mwanachuo wa CBE, Hadson Mwakilima akiuliza swali kuhusu mafao ya NSSF.
Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed akiuliza swali.
Wanafunzi wakipewa zawadi za fulana za NSSF.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akigawa zawadi ya Kalenda za NSSF kwa wanafunzi wa CBE.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Said Mohamed akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.

Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wameaswa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili wanufaike na mafao ya muda mrefu na ya muda mfupi yanayotolewa.

Hayo yalisemwa na Meneja Kiongozi wa NSSF, Eunice Chiume, kwenye semina na wanafunzi wa chuo hicho.
Aidha, katika semina hiyo, Eunice alianisha aina za mafao yanayotolewa na Mfuko huo, ambayo ni ya miuda mrefu  na mfupi.

Mafao ya muda mrefu alisema ni pamoja na pensheni ya uzeeni, kuumia kazini na fao la mazishi, ambapo alisisitiza kuwa fao la pensheni ya uzeeni ni muhimu zaidi kwa wanafunzi hao kwa kuwa watanufaika na fao hilo watakapostaafu kazi.

 Aidha, Eunice aliendelea kufafanua kwa fao la pensheni ya ulemavu mfanyakazi hulipwa  kiinua mgongo endapo ataumia akiwa kazini na pensheni ya urithi endapo kama unachangia mfuko wa NSSF ni vema akawajuza wanafamilia ili akifariki dunia warithi wa marehemu wanufaike na penshen ya urithi.

Kwa upande wa mafao ya muda mfupi, Meneja Kiongozi huyo aliyataja kuwa ni pamoja na matibabu, kuumia kazini na msaada wa mazishi.

 Kwa upande wa matibabu alisema NSSF hutoa matibabu bure kwa  mke/mume na watoto wanne kama wana miaka 18 na miaka 21 kama bado wanasoma, ambapo alifafanua kuwa watapata matibabu bure bila gharama za ziada kwa wanachama wake.

Meneja kiungozi huyo pia aliwaambia sasa shirika limekuja na huduma mpya tatu ambazo zinalenga kuwanufaisha wanachama wengi zaidi  na mafao hayo ya NSSF. Huduma hizo ni Hiyari , Mikopo ya riba nafuu na Westadi, ambapo zote alizitolea ufafanuzi.

Aidha, kwa upande wake Mkurugenzi wa wanafunzi wanaochukua shahada ya kwanza, Dk. Esther Mbise,  alisema kuwa  semina hiyo ni nzuri kwa vijana wengi  kujua  kuhusu huduma na kazi za mifuko ya jamii.

Semina hiyo iliudhriwa na wanafunzi 180 wa  CBE , wa mwaka wa tatu na wa pili,  ikilenga kutoa elimu kwao ili wajue umuhimu wa mifuko mara tu watakapoanza kujitegemea.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>