Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 3

$
0
0
KERO HII MPAKA LINI, MANISPAA YA ILALA MKO WAPI KULIONDOA?

Lori la kubeba taka likiwa limetelekezwa katika kituo cha basi cha gereji barabara ya mandela jijini Dar es salaam, na kusabaisha  harufu mbaya kwa abiria wanaotumia kituo hicho. Lori hilo lina zaidi ya siku mbili katika kituo hicho baada ya kuharibika. Manispaa ya Ilala mko wapi kuondoa kero hii?
 Uchafu uliooza na unatoa harufu kali ukiowa ndani ya lori eneo la kituo cha gereji.

Abiria wanaotumia kituo cha gereji barabara ya mandela kwa siku mbili mfululizo wamekuwa wakipata kero ya harufu kali inayosababishwa na gari ya kubebea taka iliyopaki kwenye kituo hiko.

Wakiongea na mtandao wa wetu huu wa Dj sek abiria hao wamesema kwamba gari hiyo iliharibika ikiwa inaelekea kumwaga uchafu huo na wakaisogeza kituoni hapo ili waweze kuitengeneza, lakini badala yake dereva na wasaidizi wake wakaitelekeza gari iyo toka juzi.Wakiendeleaa kuongea na mtandao wetu wamesema eneo lote la kituoni hapo linatoa harufu kali ambayo ni kero kwa wao wanaosubilia usafiri eneo hilo.
 
Mwandishi wa blog hii nilishuhudia mwenyewe na kupiga picha pia kuonja adha ya harufu kali inayotoka kwenye gari hiyo.Manispaa ya kinondoni na wasimamizi wa usafi mnaombwa kufuatilia hili na kuweza kulitatua kwani ni kero kwa watumiaji wa kituo hiki.

PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DJ SEK BLOG

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>