Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 2

$
0
0
NSSF YADHAMINI BONANZA LA MICHEZO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Maife Kapinga akimkaribisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara wakati alipotembelea banda la NSSF katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoambatana na bonanza la michezo lililofanyika DUCE jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. NSSF walidhamini bonanza hilo.
 Wachezaji  wa timu ya mpira wa kikapu ya Don Bosco wakipata maelezo kutoka kwa Maofisa Uhusiano wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo (kushoto), na Maife Kapinga kuhusu mafao yanayotolewa na shirika hilo, wakati wa bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na kudhaminiwa na NSSF.
Mshambuliaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Wanawake ya Jeshi Stars, Jabu Shaban akimiliki mpira huku akizongwa na mlinzi wa timu ya Don Bosco, Winnie Jogelea wakati wa Bonanza maalumu la maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambalo liliandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), na kufanyika jijini Dar es salaam jana. Bonanza hilo lilidhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). 
Mchezaji wa  timu ya mpira wa kikapu ya Jeshi Stars, Lucy Augustino (kushoto), akiifungia timu yake wakati wa mchezo wa bonanza lililoandaliwa na Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunuiani.
Picha za michoro zinazoonesha miradi mbalimbali ya NSSF.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>