Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(kushoto) akiwa mlezi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad akifuatiwa na Mwenyekiti wake Bibi Nasra Mohamed Halal, wengine kulia Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk,wakiwa katika Uzinduzi wa Taasisi hiyo iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hote, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)
Kikundi cha Taarab asilia cha Rahatu zamani,kikitoa burudani yao wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Bnti Saad,katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,(pichani) Muharami Mohamed,kitukuu akiimba moja ya nyimbo za Marehemu Bibi Siti Binti Saad, (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)
Picha ya pamoja.