MSIMU wa kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni, lililokuwa likisubiriwa kwa hamu hatimaye lilifanyika Juzi, wilayani Handeni Tanga ambapo kama ilivyokuwa ikitarajiwa, Shirika la Taifa la mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilijitokeza na kubeba tamasha hilo.
Meneja wa NSSF mkoani Tanga, Frank Maduga |
Shirika hilo, likiwa limejitokeza dakika za mwisho katoa udhamini wake katika tamasha hilo kubwa na la kwanza kuwahi kufanyika katika Ardhi ya wilaya ya Handeni linalojumuisha vijiji zaidi ya kumi, lilichangia fedha taslimu shilingi milioni mbili, fedha ambazo kwa kiasi kikubwa ukiacha mchango wa wahisani wengine zilichangia kufanikiwa kwa Tamasha hilo.
Akizungumza wakati wa kutambulisha wadhamini na wahisani mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo, mratibu wa Tamasha la utamaduni Handeni 2013, Kambi Mbwana alisema kukiwa na dalili zote za tamasha kushindwa kufanyika kama ilivyotarajiwa, NSSF kupitia Ofisi ya kanda ya Tanga ilijitolea kunusuru Jahazi.
Mratibu wa Tamasha la Utamaduni Handeni-Kambi Mbwana akitambulisha Wadhamini wa Tamasha hilo lililofanyika Juzi katika uwanja wa Azimio, wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. |
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu akimkaribisha mmoja wa wahisani wa Tamasha |
JKT walikuwepo wakafanya yao jukwaani ilikuwa ni noma saaaana
|
DC Muhingo Rweyemamu |
Shukurani kubwa ziende kwa NSSF, kwa kweli hawa watu wanajali utu, tunaomba watusamehe kwa mapungufu yetu lakini kwa kweli wanastahili kuitwa mfuko wa Hifadhi,” alisema Kambi
Awali akizungumza baada ya kuzindua Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kuwakutanisha watu wa Handeni kusherekea utamaduni wao pamoja na kukumbusha umuhimu wa kujenga Handeni, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kwa kuwa na Matamasha kama hayo jamii inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kupata Maendeleo wanayoyataka.
Muhingo alisema ili mafanikio yapatikane katika kila jambo ni lazima watu wa eneo Fulani wawe na utayari wa kukutana na kujadili mambo yao kwa sauti kama waratibu wa Tamasha hilo walivyofanya.
“Tunajivunia kuwa na vijana wenye mawazo mapana kama haya, naambiwa tamasha hili ni matokeo ya mawazo ya kimaendeleo ya vijana wetu, Hongereni sana,” alisema Rweyemamu.
Kwa upande wake, Meneja wa NSSF, mkoani Tanga, Frank Maduga alisema shirika hilo limedhamiria kuendelea kushirikiana na waaandaaji wa Tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha Utamaduni wa Mtanzania unatumika kulitangaza Taifa.
Mamia ya Waandamanaji wakielekea katika Viwanja vya Azimio |
Taem Tamasha la Utamaduni Handeni....chezea |