Na Janeth Jovin, TSJ
KAMPUNI ya Multichoice Africa na Afrika Media Group zimesaini mkataba wa kuonesha vipindi vya televisheni vinavyorushwa na Channel Ten.
Mkataba huo utawafanya Watanzania wote nchini kupata nafasi ya kuona vipindi vya channel ten kupitia mfumo wa digitali wa DStv.
Mkataba huo utawafanya Watanzania wote nchini kupata nafasi ya kuona vipindi vya channel ten kupitia mfumo wa digitali wa DStv.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Afrika Media Group, Ramesh Patel alisema tunajivunia ushirikiano ambao tulikuwa tukiufanyia kazi kwa mda mrefu,nafasi hiyo ambayo imeletwa na huu mkataba utakuwa na faida kwa kampuni zote vilevile kwa watamazaji wetu, haswa katika kipindi hiki ambacho Tanzania imeama kutoka mfumo wa Analojia na kuingia katika mfumo wa digitali.
Chanel ten inaubora ambao unaendana na nchi yake ingali DStv inautaalamu wa tekinolojia hii itaongeza ubora wa kuwafikia watazamaji.
Chanel ten inaubora ambao unaendana na nchi yake ingali DStv inautaalamu wa tekinolojia hii itaongeza ubora wa kuwafikia watazamaji.
Akiongezea kuhusu DStv , Mkurungezi wa Multichoice Africa, East Afrika, Stephen Isaboke alisema Multichoice inauwezo wa kuwaonyesha watu kwa masafa marefu na kwa upana zaidi kwa watazamaji wa ndani ya nchi. Ukiangalia ukuaji wa channel Ten tunaikaribisha kwenye ulimwegu wa DStv ambayo sasa imepanuka kwa channeli za Tanzania kufikia tatu ambazo ni TBc, Star Tv na sasa ni Channel ten.
Isaboke aliendelea kusema Tanzania itasonga mbele katika mfumo wa digitali, tungependa kuwahakikishia wapenzi na wateja wetu kwamba DStv ilikuwa katika mfumo wa digitali zaidi ya miaka 17 .Kwa kupitia vifurushi mbalimbali tunawazawadi wateja wetu kuchagua vipindi mbalimbali vile wanavyovipenda.
Isaboke na Petal walimalizia kwa kusema kuwa watanzania watafurahia vipindi vya Channel Ten na vipindi vya kusisimua vilivyopo DStv.
Meneja Uhusiano wa Multchoice, Barbara Kambogi (kushoto), Meneja wa vipindi wa Africa Media Group, Nicky Ngonyani (katikati) na Meneja Ufundi wa African Media Group, Augustino Mganga wakishika mikono kwa pamoja mara baada ya kusaini makubaliano yatakayowezesha vipindi vya televisheni ya Channel Ten kuonekana kupitia DStv. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Ufundi wa African Media Group, Augustino Mganga akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.
Meneja Uhusiano wa Multchoice, Barbara Kambogi (kushoto), akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.