Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 9

$
0
0
Vionjo, vyakula vya asili kupatikana ndani ya Tamasha la Handeni Kwetu Jumamosi Na Mwandishi Wetu, Handeni

BAADHI ya vyakula vya asili ya Handeni, vinatarajiwa kuwapo katika Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu 2013 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa tayari wametoa nafasi kwa wanaoweza kazi hiyo kwa umakini na usafi wa aina yake ili kuliweka tamasha hilo kwenye mguso wa aina yake.

Alisema taratibu zote zimeshafanyika ikiwamo kutembelea vikundi vitakavyotoa burudani, ambapo Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alitumia muda mwingi kuwahamasisha wadau kuhudhuria kwa wingi katika tamasha hilo, kupitia sherehe za Uhuru zilizofanyika wilayani humo Desemba 9 mwaka huu.

“Kila kitu kimekamilika, tukiamini kuwa wadau wote watakaohudhuria kwenye tamasha hilo watapata fursa ya kula vyaku7la vya asili, maana pia ni sehemu ya utamaduni wa Handeni.

“Sisi tunaamini hili ni tamasha la aina yake ambalo litashangaza watu wengi kutokana na kuandaliwa kwa kiwango cha juu, huku likianzia kwa maandamano katika Ofisi za Halmashauri ya mji Handeni kuanzia saa 2 asubuhi na kuelekea Uwanja wa Azimio,” alisema.

Kwa mujibu wa Mbwana, watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na vyakula wala vinywaji ili kudhibiti suala la afya za watu kwa kupitia tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote, hususan wapenzi wa utamaduni hapa nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>