Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19278 articles
Browse latest View live

Article 0

$
0
0

Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana,Wanawake na Watoto

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana,Wanawake na Watoto, katika utekelezaji wa Mpango wa kazi za Wizara hiyo, katika  Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman Ikulu).

Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa Wizara ya  Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, wakiwa katika mkutano wa  utekelezaji wa Mpango wa kazi za Wizara hiyo, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. AliMohamed Shein, (hayupo pichani)  katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman Ikulu)


Article 3

$
0
0
WATEJA WA SKYLIGHT BAND WABURUDISHWA NA MOKAI BIA Wateja wa Skylight Band wiki iliyopita walipata nafasi ya kuburudika na kinywaji kipya kabisa toka nchini Sweden MOKAI Cult ambacho kina Alcohol 4.5 yenye ladha murua kama aina ya Savanna ambacho ni zaidi ya Savanna.

Hakika wateja wa Skylight Band katika ukumbi wa Thai village Masaki wiki iliyopita walichangamka kweli na kinywaji hiki toka huko Sweden chenye Alchohol ya wastani ambayo mtu anaweza kumudu kunywa na kuamka safi kabisa bila Hang-Over.
DSC_0412
Mashabiki wa Skylight Band wakiingia getini walipata fursa ya kuonjeshwa kinywaji hicho kipya kutoka Sweden kinachotambulika kama MOKAI Cult ambacho kitakuwepo kila siku ya Ijumaa ndani ya Thai Village jijini Dar na kuzidi kuwachangamsha mashabiki wa Bendi hiyo kusakata Rhumba zaidi.
IMG_5171
Mrembo wa MOKAI Cult akifafanua jambo kwa wateja juu ya kinywaji hicho kipya.
IMG_5164
Mbunifu wa Mavazi Gabriel Mollel akiuza sura na Models Neema Mbuya pamoja na Anna.
IMG_5181
Miss Tanzania 2011 Salha Israel (wa tatu kulia) kwenye picha ya pamoja na marafiki zake ndani ya Thai Village-Masaki jijini Dar Juma lililopita.
DSC_0393
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakipata Ukodak na Warembo wa MOKAI Cult waliokuwa wakaribu kwa wateja na kutoa huduma yenye kiwango cha kimataifa. Njoo wewe na yule leo tujikoki na MOKAI.
DSC_0418DSC_0431IMG_5141
Rappa wa Skylight Band Joniko Flower akiongoza makamuzi na kikosi kazi cha band hiyo kutoa burudani kwa mashabiki wake Ijumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa Thai Village jijini Dar.
IMG_5187
Divas wa Skylight Band wakiongozwa na Aneth Kushaba AK47 katika burudani ya aina yake yenye kiwango cha kimataifa kwa mashabiki wake.
DSC_0006
Digna Mbepera akikamua jukwaani huku akipewa Back-Up na Mary Lucos pamoja na Winfrida.
DSC_0044
Wo! I feel good, I knew that I wouldn't of.....I feel good, I knew that I wouldn't of.....So good, so good, I got you......Joniko Flower, Aneth Kushaba sambamba na Irene binti mwenye kipaji cha kutumia "Saxophone" .
DSC_0034
Irene akipuliza Saxophone.
DSC_0018
Mchaka mchaka mwanzo mwisho hapa chezea Skylight Band.
DSC_0030
Mzuka ukiwa umempanda Sam Mapenzi wa Skylight Band.
DSC_0068
Mdau Alois Ngonyani kama kawaida yake hakubali kushindwa.....!
DSC_0098
Warembo wa MOKAI na miondoko ya "Yachuma Chuma".
DSC_0108
Joniko Flower akitangaza zawadi kwa mtu atakayecheza vizuri atajishindia chupa mbili za MOKAI.
DSC_0121
Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band akijimwaga jukwaani kuonyesha umahiri wake.
DSC_0129
Na mwishowe alikabidhiwa zawadi ya chupa mbili za MOKAI pamoja na kupata Ukodak na warembo wa kinywaji cha MOKAI Cult.
DSC_0143
Zawadi ziliendelea kugawiwa kama inavyoonekana pichani.
DSC_0156
DSC_0160
Bado nimo kumbeeee.....!...Wababa nao hawakubaki nyuma kwenye burudani.
DSC_0117
Wadau wetu wa ukweli wakipata Ukodak.
DSC_0015
Dk. Sebastian Ndege akishow love na mmoja wa marafiki zake kutoka Mwanza.
DSC_0180
Hapo vipi?? Bata mwanzo mwisho na MOKAI halali mtu hapa mpaka kieleweke.
DSC_0395
Familia ya Skylight Band.
DSC_0400
Wadau wakifurahia Ukodak.
DSC_0063
DSC_0439  IMG_5125
Shika Moyo.......x3........Warembo wa MOKAI wakicheza sebene la Skylight Band.
DSC_0403

Article 2

$
0
0

MARUFUKU BONGOWOOD, SWAHILIWOOD

Na Andrew Chale, Arusha

WAAFRIKA wametakiwa kukataa utumwa na kuiga  neno la ‘WOOD’, kwenye soko la filamu hasa baada ya nchi nyingi kukopi  jina la ‘HOLLYWOOD’ ambalo ni eneo lililopata umaarufu mkubwa kwenye soko la filamu Duniani kwa kuwa na wasanii nyota na studio za kisasa, za masuala ya filamu.

Akielezea mapema leo kwenye semina ya waandishi wa habari za Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, Mkurugenzi wa Tamasha la Filamu za Kiafrika la  Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia,  kilichopo Pensylvania, Marekani , Mr. Akpor Otebele,  alisema Waafrika waache dhana ya kuendelea kutumia jina hilo ambalo nchi nyingi wamekuwa wakitumia  viunganishi vya neon hilo la ‘Wood’  bila kujua maana hasa la kuendelea kulitumia.

Hii aina maana, ni la kuliacha na Nigeria kule waigizaji wengi wanatafakari maana ya hili neno lakini jibu hakuna, lakini bado wanaendelea kulitumia” alisema.

Akitolea mfano wa baadhi ya nchi zinazotumia jina hilo kutoka Hollywood, ni pamoja na : Bongowood/ Swahiliwood (Tan zania), Nollywood (Nigeria), Riverwood (Kenya), Ghollywood (Ghana), SierraWood (Sieralion)na Congowood (Kongo) na mengine mengi.

Akpor  Otebele aliongeza kuwa, kuendelea kutumia viunganishi hivyo ni kuwanufaisha watu wa Magharibi na kuupamba Mji wa Hollywood  unaoishi mastaa na studio maalufu huko Lose Angels nchini Marekani, ambapo kwa dhana hii inafanya Waafrika kuwa watu wasiojua wanachokifanya.

…”Swahiliwood, its means, Swahili ubao? Is  that sure? So why to use ‘Wood’??  in Swahili mean ‘UBAO’?? Alisema Akpor Otebele.

Na kuongeza kuwa  nchi nyingi za Afrika zinatumia neno
'Wood' kinyume na maana yake  huku wengine wakipokea misaada bila kujijua kuwa wanarubuniwa ujinga. "Kwa nini wanahitaji Bongowood. Mimi ninavyojua wood ni mbao, kwa nini wasiseme, swahili movie?" alihoji.

Otebele aliwataka wanahabari  kuwaelemisha wadau wa filamu kuwa, Hollywood si jina la kutungwa bali la mji uliotokea kuwa maarufu kutokana na kusheheni vitendea kazi bora na vya kisasa na kwenye makazi  ya wasanii nyota mbali mbali, ni wakati wa kulipinga.

Mbali na hilo, Otebele  aliwataka wasanii na waongoza filamu Afrika na kwingineko kuzingatia  filam,u za kiushindani ilikufia malengo yao.

Hii ni kwa  kuwataka kuzingatia filamu zenye ubora, maarifa na zitoazo mafunzo mbele ya jamii inayotuzunguka kila siku.

Katika semina hiyo inayofanyika  jini hapa,  katika hoteli ya  kisasa na kitalii ya Silver Palm Hotel,  ambapo mada mbali mbali zitawasilishwa kuhusu tasnia ya  filamu barani Afrika huku  watoa mafunzo wengine wakiwemo Mtaalamu wa filamu wa chuo kikuu Mlimani, ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu ya ‘CHUNGU’,  Shule  na  Mtendaji Mkuu wa ZIFF, Prof. Martin Mhando.

Semina hiyo ilianza mapema leo inatarajia kuendelea  hadi Desemba Mosi,  huku ikiandaliwa na Waandaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Majahazi (Zanzibar International Films Festival –ZIFF)  kwa  udhamini wa Mfuko wa kusaidia Vyombo vya habari nchini  (Tanzania Media Fund-TMF)  ambapo  waandishi mbali mbali wanapatiwa mafunzo juu ya uandishi wa habari za Sanaa hapa nchini kwenye vyombo vyao vya habari na mitandao ya kijamii zikiwemo blogs.

Pia semina hii inaendana na tamasha kubwa la filamu  la AAFF 2013, lililoanza  Novemba 25 hadi Desemba Mosi, kwenye  kumbi mbali mbali za Alliance Francaise, Via Via , Mount Meru Hotel, Mango Tree & New Arusha Hotel, ambapo kiingilio ni BURE/FREE ENTRY.

Article 1

$
0
0
Wanakijiji 800 wayakimbia makazi yao kwa kuofia kupigwa na Polisi

Na Kenneth Ngelesi, Mbarali

ZAIDI wa wanakijiji 800 kutoka kitingoji cha Magwalisi kijiji cha Nyeregete Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, wameya kimbia makazi yao baada ya kuvaniwa na wenzao wa kutoka vitongoji sita vya kijiji hicho wakiwa na mikuki,mpanga na silaa zingine za jadi kwa lengo la kuyanyang’anya mashamba yao ili wagawane.

Wanakijiji hao wamefikia hataua hiyo baada ya watu hao ambao sehemu kubwa walikuwa ni vijana kutoka vitongoji hivyo  vya kijiji cha Nyeregete walisadiwa na jeshi la Polisi kutoka kituo cha  Rujewa ambao walifika katika Mtaa huo na kuanza kuvunja milango ya vyumba  kadhaa ambapo nyumbani  5 zilichomwa na kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea Novemba 26 mwaka huu majira ya 10:00 jioni mawaka huu, na kwamba Mkuu wa wilaya hiyo Gulamhussein  Kifu ndiye anaye daiwa kuwa  kinara wa mpango huo wa kupora mashamba akishikiana baadhi ya wafanyabiashara Mazar Juma  kutoka katika mji wa Rujewa na Mwandulami kutoka  Mkoani Njombe ambao wanafadhili mgogoro huo.

Akisimulia Mkasa huo kwa waandishi wa habari waliofika katika eneo la tukio, mwanakijiji ambaye ni muhanga wa tukio hilo aitwaye Mkima Luhende kutoka kitongoji hicho alisema kuwa siku ya tukio Polisi kwa kushikiana na vijana  80 kutoka katika vitongoji sita ambavyo ni Lyahamile,Tembo A na B,Simba,Nyati,Nyaluanga,walifika kwenya mashamba yao  na kuanza kupima  kwa  lengo la kuayagawa kwa kila aliye kuepo katika eneo hilo.

Baada ya kuanza kwa zoezi hilo  Luhende alisema kuwa waliamua kusimama kila mmoja katika shamba lake kwa lengo la kuzuia zoezi hilo lisiendelee na ndipo walipoanza kushushiwa kipigo na wavamizi hao waliyo kuwa wakisadiwa ba jeshi la polisi ambao walikuwa wakipiga mabomu kwa lengo la kuwa ogofya wakulima.

Akizungumza kwa uchungu Luhende alisema kuwa baada ya kushushiwa kipigo hicho, waliamua kukimbia makazi yao na ndipo polisi kwa kushirikiana na vijana wa Nyeregete walipoanza kuvamia makazi yao na kupora vita mbalimbali zikewemo fedha taslimu sh mil 2 .

Luhende aliongeza kuwa mbali na kuchukua kiasi hicho cha fedha, wavamizi hao pia walipora, betri tatu za gari,magania,10 ya mpunga,kuku  20, simu zisiozo na idadai ambazo zilikuwa zinachajiwa,seti ya makochi pamoja na mito yake.

Hata hivyo Luhende ambaye ni mmoja watu ambao mashamba yana windwa na wahusika hao ambaye anamiliki ekari 20, alisema ni muendelezo wa kuwa nyanyasa watu wa jamii ya kisukuma wanaoishi katika Wilaya ya Mbarali na kumiliki ardhi kwani kitongoji hicho ndicho pekee kina kaliwa na watu wa jamii hiyo.

Mkulima mwingine aliye patwa na mkasa wa kuporwa mali ni Nkuba Mahalu alisema kuwa wavamiwa hao walifika nyumbani kwake na kupora gunia kumi za mpunga na seti moja ya kochi, kabla ya kuhamia kwenye nyumba ya mwanamke aitwaye Johari Mohamed ambaye walifanyia vurugu kabla kabla kuchukua begi lake la nguo ambalo ndani yake  kulikuwa na sh 800,000/ na kubomoa vienge vya mahindi na kisha kumwagia maji.

Mbali huyo mwanamke mwingine katika kitongoji hicho Kwangu Deus anadiwa kupotelewa na watoto sita ambao walikimbia  baada ya uvamizi kufuatia kelele za mabomu, na kwamba mpaka waandiashi wanaondoka eneo na tukio Novemba 28 majira ya saa 12:jioni mwaka huu walikuwa hawajulikana walipo akiwemo mumewe na watoto wengine wa mjirani.

Hata hivyo baadhi ya wanakijiji walio zungumza na waandishi wa habari walidai kuwa mpango huo wa   kuporwa ardhi, unaratibwa na Mkuu wa wilaya hiyo Kifu kwa kuwatumia vijana hao ili waipole ardhi ili baadaye wagawe kwa wafanyabiashara hao.

 “Ndugu zangu wana habari ni vema mkafamu kuwa mpango huu wa kupora ardhi yetu unaratibiwa na mkuu wetu wa wilaya, akishirikiana baadhi ya watendaji kutoka mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa kwani sisi ndo watu wa kwanza kutoa taarifa kwake lajkini hakuna hatua zozote alizo chukua”,alisikika mwananchi mmoja
Walisema kuwa kitu kingine kinacho fanya waamini kuwa mpango huo upo chini ya Mkuu huyo wa wilaya ni kwamba mbali  kufanyiwa uvamizi huo lakini bado jeshi la polisi kituo cha Rujewa kina washikiria  wananchi 12 na watoto 4  chini ya miaka 14  kutoka katika kitongoji hicho ambao kimsingi ndiyo waliyo fanyiwa fujo.

Walisema kuwa katika hatua niyingine vitu walivyo kuwa wakiporwa vilikuwa vinasombwa kwa kutmia magari ya Polisi yaliyo kuwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kuwasomba wanachi hao ambao hata hivyo wengi wao wamekimbia makazio yao kwa zaidi ya siku tatu kwa kugopwa kukamatwa na polisi nanyo ni kuku,mahaindi na magodoro,.

Wogo wawa wanchi hao ulidhirishwa wakati gari la waandishi likiwasili katika kitiongoji wengi wao walianza kukimbia lakini juhudi za wenzao wal;ianza kuwa p9gioa siomu wakiwa taka kurejea katika makazi yao kwani gari lilikuwa limewabeba waandishi wa habari na si maadui zao.

Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SSP Diwani Athuman akizungumzia suala hilo alithibitisha kuwa na taarifa za tukio hilo,na kwamba jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi.
Aidha Diwani aliongeza kuwa katika tukio hilo ni kwamba taarifa alizopewa na OCD wa Mbarali zinasema kuwa mpaka jana jioni watu kumi ndiyo walikuwa wanashirikiliwa na jeshi polisi kituo cha Rujewa.

Kamanda huyo wa Polisi alikiri kuwa mgogoro huo unachochewa na Mkuu huyo wa wilaya na kwamba wananchi wa kitongoji cha Magwalisi wanaonewa kwani ardhi hiyo wana miliki kiharari kuanzia mwaka 1973 walipo hamia katika eneo hilo.

Hata hivyo mara baada ya kutoka eneo la tukio waandishi wa habari walitamtafuta Mkuu huyo wa wilaya kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi juu ya suala hilo,lakini simu yeke iliita bila kupokelewa, na baadaye kutopatikana baada ya kuzimwa.

Article 0

$
0
0
KASEBA,ALIBABA KUZIPIGA  FRIENDS CORNER HOTEL

Mabondia Japhet Kaseba na Alibaba Ramadhan wa Arusha wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21 Desemba 2013 katika ukumbi wa friends corner hotel.
Pambano hilo liloandaliwa na Ibrahim kamwe chini ya  BigRight promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi likiwemo la ubingwa wa mkoa kati ya karage suba na bondia mkali anaechipukia kwa nguvu  Fadhili awadh[tiger]  katika uzito wa wealter '66kgs' pambano la raundi kumi.

Akizungumza na vyombo vya habari mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe alisema zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa,pia mahasimu wawili wa uzito wa juu lusekelo Daudi atazipiga na  Mbaruku kheri (ndota) katika marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi. 
Nae Adam yahaya 'Baby Edo' atazipiga na Harman Richard, mkongwe Enerst Bujiku 'tyson' atacheza na shah kasimu kukumbushia Enzi za akina Stanley mabesi, jocky hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena rajabu, nae  issa omar  atazipiga na haji juma wa Tanga, moro best atapigana na shafii ramadhan, huku Shaban Bodykitongoji akizipiga na mwinyi mzengera. 
Mabondia wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huona wameshaingia kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi toka kiwango security na jeshi la polisi

Article 0

$
0
0
Viingilio Tamasha la Krismas vyatajwa

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha la Krismas wametangaza viingilio vya tamasha hilo ambavyo kima cha chini ni shilingi 5000.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama viingilio vingine viti vya kawaida, 10000 VIP B na VIP A 20000.
Msama  alisema watoto katika tamasha hilo watachangia shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa jamii kujipanga kwa ajili ya tamasha hilo.

Aidha Msama alisema viingilio katika mikoa yote litakakofanyika ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000na kuendelea kueleza kwamba wadau wajipange vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo. 

“Tunafanya taratibu za tiketi za tamasha hilo ambazo tumepanga zitoke Uingereza, ili kukwepa wizi utakaofanywa na baadhi ya wasiolitakia mema,” alisema Msama.

Msama alisema wanajipanga vilivyo kuhakikisha wanakomesha ujanja unaotarajia kufanywa na wasiolitakia mema tamasha hilo ambalo dhamira yake ni kusaidia wanaoishi katika mazingirahatarishi wakiwemo yatima, wajane na walemavu.

 Waimbaji katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu na New Life Band (Tanzania) na waimbaji kutoka nje ya Tanzania ni pamoja na Solly Mahlangu, Liliane Kabaganza, Solomon Mukubwa na Eiphraim Sekeleti. 

Article 9

$
0
0
EMMANUEL MSUYA AIBUKA MSHINDI WA EBSS 2013

 Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2013, Emmanuel Msuya (kati) akishukuru Mungu baada ya kutangazwa kushinda zawadi ya milioni 50 za shindano hilo lililodhaminiwa na Zantel. Kulia ni mshindi wa pili, Elizabeth Mwakijambile na  Ofisa Mkuu wa Fedha wa Zantel, Ali Bakari.
 Msuya akiangua kilio cha furaha baada ya kutangazwa mshindi.
Msuya akiangua kilio cha furaha baada ya kutangazwa mshindi.
Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Maina Thadei na Melisa John.
Maina Thadei.
 Walioingia tatu bora.
Mshindi wa Epiq Bongo Star Search, Emmanuel Msuya akiwa na mshindi wa pili wa shindano hilo, Elizabeth Mwakijambile kabla ya kutangazwa kwa mshindi wa shindano hilo. 
 Mshindi wa pili wa shindano la Epiq Bongo Star Search, Elizabeth Mwakijambile akiwajibika jukwaani.


Emmanue Msuya.
 Amina Chibaba.
 Mshindi washindano la Epiq Bongo Star Search, Emmanel Msuya akiwajibika jukwaani.
Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search, Emmanuel Msuya wa jijini Mwanza (katikati), akipokea kitita cha sh. milioni 50 kutoka kwa jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen baada ya kuwashinda washiriki wenzake watano walioingia katika fainali hizo. Wa pili kulia ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa Zantel, Ali Bakari 
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel  
 Mashabiki wakifuatilia fainali hizo.
 Majaji.
 Emmanuel Msuya.
Wasanii wakitoa burudani.
Barnabas Elias 'Barnaba' wa THT akitumbuiza. 
Melisa John.

  Emmanuel Msuya.

Na Elizabeth John

 Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.

Emmanuel Msuya wa jijini Mwanza, jana usiku aliibuka mshindi wa Epiq Bongo Star Search (EBSS) kwa mwaka huu baada ya kuwabwaga wengine wanne waliofika hatua ya fainali, hivyo kutwaa kitita cha shilingi milioni 50.

Msuya aliibuka kidedea katika fainali hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na kupambwa na wasanii mbalimbali wakiongozwa na mkali kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (THT), Elias Barnaba ‘Barnaba Boy’.


Mbali na kuondoka na fedha hizo, Msuya atapata mkataba wa kurekodi nyimbo zake katika studio ya MJ rekodi inayomilikiwa na Jaji wa mashindano hayo, Joachim Kimario ‘Master Jay’ pamoja na kukatiwa bima ya afya ya kutibiwa mwaka mzima.


Msuya aliwabwaga washiriki wengine walioingia fainali, Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Maina Thadei na Melisa John.


Nyota huyo aliibuka kidedea baada ya kuimba kibao cha ‘Maneno maneno’ kilichoimbwa na mkali wa muziki wa RnB nchini, Bernard Paul ‘Ben Pol’ ambapo pia mshindi wa mwaka jana, Walter Chilambo aliondoka na kitita hicho baada ya kuimba wimbo wa msanii huyo unaojulikana kwa jina la ‘Nikikupata’.


Jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen ‘Madam Ritha’ alisema ili mshiriki aweze kuibuka mshindi anatakiwa kujiamini anapokuwa jukwaani na kuweza kulimiliki jukwaa vizuri.


“Vigezo tunavyoangalia kumpa ushindi, mshiriki anatakiwa kuwa na imani na anachokifanya, umahiri wake wa kuimba anapokuwa jukwaani, pia huwa tunamshauri mshiriki kuimba wimbo ambao anaufahamu vizuri,” alisema Madam Ritha.


Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Msuya alisema yeye hajui ni kitu gani kimempa ushindi huo yote anamuachia mungu.


“Kiukweli siwezi kuzungumza lolote kwani nina furaha ya ajabu, mimi sijui lolote najua mungu alikuwa na mimi pia nawashukuru sana majaji wangu pamoja na Watanzania wote ambao walikuwa wananipigia kura,” alisema.


Mbali na Barnaba, wasanii wengine waliopamba fainali hizo ni pamoja na msanii chipukizi wa hip hop, Kimbunga, Young Killer ‘Msodoki’, Makomandoo, Snura na Shaa.


Shindano hilo kwa mwaka huu limedhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Zantel pamoja na Salama Kondomu.


Article 8

$
0
0
TAMKO LA UMOJA WA MATAWI YA WANACHADEMA MKOA WA MWANZA DHIDI YA UAMUZI
.
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTANGULIZI

Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi wa matawi 189 ya chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa mwanza. Umoja huu wa matawi unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.

Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30.nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wetu wanaotuwakilisha kwenye vikao vya maamuzi kama vile wilaya, mkoa na taifa wamekuwa waoga na wameshindwa kuwakilisha mawazo yetu tuliyowatuma badala yake wengi wao wamekubali kuwa vibaraka wa kile kinachoitwa CHADEMA KASKAZ

Kutokana na ukweli kwamba msingi wa chama chetu na chama kingine chochote kile cha siasa, uimara na uhai wake unatokana na uwepo wa misingi na matawi ya chama, hivyo sisi wanachama wa matawi haya 189 tumeamua kuunganisha nguvu zetu kutetea chama chetu na kuhakikisha haki, heshima, katiba na maadili ya chama vinafuatwa bila ya kuogopana wala kuoneana haya.
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-

Chadema ni chama cha siasa kinachopaswa kuendeshwa kwa misingi ya kufuata taratibu, kanuni na katiba yake na si vinginevyo. Lakini badala yake kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa juu kujitwalia mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama chetu hususan katika kutoa haki sawa kwa viongozi na wanachama wa chama chetu. Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya juu sana kwa wale wanao amini kuwa ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo kupelekea kuwaadhibu kama ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza bila kuhojiwa au kukosolewa.



Sababu zilizotolewa na kamati kuu hazikubaliki

Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe 20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi KabweDr. Kitila Mkumbo na Ndg Samson Mwigamba, kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali ni unafki na Uzandiki wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa Demokrasia kwa kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama. Katiba yetu imeweka wazi Ibara ya 6 Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za nidhamu na uwajibishaji ndani ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi bila kufuata taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo sisi baadhi ya wanachama huo ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi wetu waliotumia nguvu zao na akili nyingi sana kukijenga chama.

Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni

1.    Kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za serikali.
2.    Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.

3.    Harambee  za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
4.    Kutaka kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.

5.    Kutaka kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.
Kushamiri kwa migogoro

Mwenyekiti na katibu mkuu wameshindwa kutatua migogoro ya viongozi na wanachama kutoka mikoani kwa njia sahihi za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa viongozi na wanachama kutumia njia ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na katibu mkuu mwenyewe, kujitokeza mara kwa mara kwenye mitandao hiyo hiyo kwa madai ya kutolea ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya husuyo maswala ya chama ilihali akijua kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao ilipelekea migogoro mikubwa sana hususan mkoa wetu wa Mwanza na kupelekea kupoteza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya chama na kutumia nafasi zao kuopanga safu za uongozi wanao uwona watawatumikia wao na si chama, hivyo kusababisha mifarakano mikubwa ndani ya chama na kupelekea kuvuliwa uongozi kwa viongozi mbalimbali katika mkoa wetu kwa maamuzi yasiyo zingatia utafiti na uhalisia wa kweli ndani ya chama.

Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja katiba Mfano:

·        Kitendo cha kutoa muongozo nje na matakwa ya katiba juu ya kuwapata wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama wabunge kwamba wanaohitaji kugombea 2015 waandike barua makao makuu na wao ndio watatoa wagombea kinyume na katiba ya chama Ibara 7.2.13 inayotoa taratibu ya kuwapata wagombea, huwo ni uvunjaji wa katiba na ubakaji wa demekrasia ndani ya chama, sizani kama kuna uhaini zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama leo sisi Chadema hatuheshimu katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje siku tukikabidhiwa nchi yenye watu wenye mawazo na mtizamo tofauti na sisi?. Hatutaki kuamini kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja wa maopambano ya kivita.

Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lemakumkashfu kiongozi wa chama Mh: Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na Mzandiki kwendye mitandao ya kijamii pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw Henry Kilewo kwa kuweka  waraka unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu Zitto mbao chama makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama kukana mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo chama hakiusiki nao na hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw Kilewo ambaye pia ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama, waraka huo ambao chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali akijua kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu maadili ya viongozi kanuni ya 10.

Pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa kwa waandaaji wa tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti ya siri kuhusu Zitto kwasababu tayari makada na viongozi wetu wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni mwa waandaaji wa tamthilia hii.

Lakini cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia macho na kupelekea kwetu baadhi ya wanachama kuamini zengwe hili la kumchafua Zitto Lina Baraka zote za viongozi wa chama ngazi ya juu.

Tunataka kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa waraka ujulikanao kama mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo itumike kwa hawa waliotumia njia chafu ya kuandaa waraka wa kumchafua zitto ambao chama kinawajua na baadhi yao tumewaweka humu kwenye tamko letu.

Kingine tunataka kwa mara nyingine kwa viongozi wa chama makao makuu kuwaambia umma wa watanzania ni kwanini waraka huo huo uinaoitwa warajka wa siri kuhusu Zitto leo viongozi na wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka huo uangawiwa kwa wanachama na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si ubaguzi ni nini?.

Tunaonya na kulaani kitendo cha viongozi wetu kuendeleza utawala wa kibabe na kupelekea kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanachama na viongozi wanaotofautiana nao kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya baadhi ya viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja jukwaani hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia maneno ya uchochezi dhidi ya wanachama na viongozi wanaokinzana nao kifikra na kimtizamo na kuhamasisha wanachama wasiojua itikadi vizuri ya chama kuwa wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa hadharani kwenye mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli kubaki na maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali kuhusiana na jambo hili.

Hitimisho
Mwekiti na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii,  M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.

Mwisho tunataka maamuzi haya HARAMU kamati kuu yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na wapigania Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka uongozi uliopo
  utoke madarakani.

Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.

Tunamuagiza mbowe na slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu,
Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha,
Sasa sisi wanachadema wa matawi ya mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi watupo chadema kwa bahati mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi wakuu wa chama hiki, tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob Nyanga Makani, Marehemu Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, kamanda Zitto Kabwe na sisi wengine wengi.
Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA. 

Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA

ROBERT E. GWANCHELE
Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA

0757 084776

Article 7

$
0
0
MSAMA ATOA MSAADA KITUO CHA YATIMA LUHILA PACHANE MKOANI RUVUMA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions, Alex Msama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions, Alex Msama, amemkabidhi msaada wa magodoro yenye thamani ya sh. milioni 4.5 mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Luhila Pachane kilichopo Songea mkoani Ruvuma, Sheikh Abdushakur Omary. Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

Na Francis Dande


MKURUGENZI Mtendaji wa Msama Promotions, Alex Msama, amekabidhi msaada wa magodoro yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 4 kwa kituo cha watoto yatima Luhila Pachane kilichopo Songea mkoani Ruvuma.


Akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi za Msama Promotions, Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, Msama alisema msaada huo umetoka kwenye Mfuko wa Tamasha la Krismasi ambalo linatarajiwa kuanza Desemba 25 jijini hapa na mikoa mingine.


Tamasha hilo linatarajia kufanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Arusha na Dodoma.


Msama alisema kuwa kutokana na maombi ya kituo hicho na kuguswa na hali waliyokuwa nayo ya yatima hao kulala katika mikeka, aliamua kunyofoa sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye Mfuko wa Tamasha la Krismasi na kuwasaidia watoto hao ili nao waweze kujisikia wapo katika jamii ya Watanzania.


“Nimeamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na hali halisi waliyonayo yatima hao wa kituo cha Luhila Pachane huko mkoani Ruvuma, nikaamua kunyofoa fedha katika Mfuko wa Tamasha la Krismasi kwa ajili ya kuwasaidia ili nao wajisikie wako pamoja na Watanzania wenzao.


“Msaada huo wa magodoro hayo ni zaidi ya shilingi milioni 4, hivyo nina imani kubwa sasa kwa msaada huu yatima wataniombea kwa Mungu ili Tamasha la Krismasi liwe la mafanikio, kwani lengo la tamasha hilo ni kuweza kujenga kituo cha kisasa cha watoto yatima na wasiojiweza, kwani kiwanja tumeshakiona kipo pale maeneo ya barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam,” alisema Msama.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo, mlezi wa kituo hicho ambaye pia ni Katibu wa Bakwata Mkoa wa Ruvuma, Sheikh Abdushakur Omary, alimshukuru Msama kwa wema wake aliouonyesha wa kusaidia jamii ya Watanzania wote bila kubagua dini, kabila wala rangi.


“Msama ni mtu wa aina yake, hana ubaguzi, anashughulikia maombi ya Watanzania wote bila kuangalia dini, kabila, rangi wala utaifa wake, kwani anaamini kuwa wote ni wamoja, hivyo naomba tuzidi kumuombea aendelee kuwa na moyo huo wa kujitolea kwa ajili ya watu wa taifa lake wasiyojiweza,” alisema Omary.


Hata hivyo, aliomba wizara husika kuharakisha upatikanaji wa hati ya kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kutolea misaada (Center) cha Pugu.


“Uwepo wa Msama katika ulimwengu huu kunamuwakilisha Mwenyezi Mungu, kwani Mungu si mbaguzi kwa watu wake, anawapenda wote na anatoa sawa kwa kila mtu, hivyo ndivyo alivyo Msama, kwa moyo mmoja namuombea yeye na taasisi yake isiyokuwa na ubaguzi wa dini kuendelea kuwa hivyo wakati wote,” alisema Omari.

Article 6

$
0
0
KOCHA WA SIMBA ATUA DAR KURITHI MIKOBA YA KIBADENI
 Mashabiki wa Simba wakimlaki kocha mpya wa timu hiyo, Zdravko Logarusic, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, akitokea Croatia. (Picha na Francis Dande)

Karibu Msimbazi!!

Article 5

$
0
0

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHEREHESHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM, LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, wakati  alipotembelea katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA, katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na yeye kuzaliwa salama. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya  Jukwaa Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye  maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es 
Salaam, leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid, (wa pili kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akimkabidhi mija kati ya Vitabu vya Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), 
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Mussa, baada ya ya kuzindua mpango mkakati huo wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi, Mashine za CD4 kwa ajili ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha na OMR)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.

Article 4

$
0
0

MALORI YAGONGANA NA KUZIBA NJIA ENEO LA WAMI

 Malori yaliyogongana yakiwa yameziba njia baada ya kugongana eneo la mto wami
 Foleni ni kubwa sana ya mabasi yaendayo mikoa ya Tanga,Arusha Na Kilimanjaro.
Ajali mbaya imetokea mda huu eneo la mto wami na kusababisha Foleni kubwa sana kwa magari na mabasi yanayotumia njia hiyo, Dj sek blog imefanikiwa kupata picha kadhaaa za ajali hiyo,Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli breki kwa malori hayo yakiwa yanateremka kwenye mlima huo.Polisi wanaendelea na jitihada za za kuyatoa ili njia ipatikane kwa ukubwa zaidi ili kuruhusu upitaji mzuri wa magari.

Article 3

$
0
0
WAFANYAKAZI TBL WASHIRIKI KUPIMA KWA HIARI VIRUSI VYA UKIMWI
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Tereza Mbando (katikati), akiwasha mshumaa kuzindua zoezi la kupima virusi vya ukimwi kwa hiari kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani. Kulia ni Meneja Raslimali watu wa kampuni hiyo, Bw. David Mafuru.
 Muuguzi Mshauri wa kupima maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Bi. Aulelia Kunambi, akimpima Meneja Raslimali Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. David Mafuru (kulia), wakati wa zoezi maalumu la kupima Ukimwi kwa hiari kwa wafanyakazi wa Kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa baada ya kushiriki katika zoezi la kupima ukimwi kwa hiari, wakati wakiadhimisha siku ya Ukimwi Duniani.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa baada ya kushiriki katika zoezi la kupima ukimwi kwa hiari, wakati wakiadhimisha siku ya Ukimwi Duniani.
Wasanii wa kundi la THT wakitoa burudani kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, wakati wa zoezi la kupima virusi vya ukimwi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Dar es Salaam

Article 2

$
0
0
Askofu Mshana; Msimseme Yesu mdomoni
 Familia zilizobariki watoto Mshoto mwenye Suti Nyeusi ni Mchungaji Naftari Njavike wa KKKT Mnadani Dodoma.
Kwaya Paradiso Mnadani KKKT ikionyesha Umahiri wa Uimbaji.

Na Bryceson Mathias, Mnadani Dodoma


WAKRISTO kote nchini, wametakiwa kutomsema Yesu Kristo mdomoni na badala yake wamthibishe na kumsema kwa Mawazo, Maneno na Matendo moyoni mwao, kwa sababu ni hakika Yesu anakuja kama alivyoahidi asitukute tunatangatanga.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Samweli Mshana, katika Ibada ya Sakramenti ya Kipa Imara iliyofanyika Usharika wa Mnadani, Jimbo la Makao, ambapo wahitimu 33 walibarikiwa.

Akihubiri katika Ubarikio huo Jumapili iliyopita [Desemba 1, 2013], Mshana aliwatahadharisha Wakristo kwamba, hawana sababu ya kumtaja Yesu midomoni mwao tu, bali wamdhihirishe mioyoni mwao kwa Mawazo, Maneno na Matendo, kwa kuwa ni hakika Yesu anakuja kama alivyosema.

“Ni Ukweli usiopingika Dalili zote za kurudi kwake zionekana kama alivyosema, hivyo hatuna sababu ya kuwa kama watu tusiojua alichosema, bali tunatakiwa kukaza macho na mioyo yetu kwake, ili tuje tumraki mawinguni tufurahi naye”.alisema Askofu Mshana.

Alilionya Kanisa (Waumini) na Wazazi na Taifa kwamba, Watoto wetu wa sasa hivi wanajua mambo mengi kuliko enzi yao kwa sababu ya Changamoto za Ki-Utandawazi, hivyo akatoa wito Kanisa, Wazazi, Jamii na Viongozi wa Taifa kutobweteka ila waombe kizazi hiki kisiharibiwe.

Mbali na Ibada ya Kipa Imara, Askofu Mshana alichangisha Shilingi Milioni 1.4/= kwa ajili ya Ujenzi wa Hostel ya Usharika huo (KKKT Mnadani) unaoongozwa na Mchungaji Naftari Njavike, Hostel ambayo ilikuwa imesimama kwa miaka kadhaa ili kupisha shughuli zingine za maendeleo, lakini kwa sasa ipo kwenye Lenta.

Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi wa Usharika huo (Njavike), alimshukuru Askofu Mshana, Wazazi wa waliobarikiwa, Baraza la Wazee, Waumini na Watoto hao, kwa kufanikisha kuongeza Idadi ya Wakristo wapya yakiwemo Mafanikio ya Harambee ya Ujenzi wa Hostel.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na Wachungaji wa Jimbo la Makao Makuu, Watumishi na Watendaji wote wa Dayosisi ya Dodoma, ambapo ilinogeshwa na Kwaya ya Usharika Mnadani na ya Paradiso, ambazo zilitumbuiza na kuboresha Sherehe Ibada hiyo.

Article 1

$
0
0
MKUTANO MKUU WA ISSA WAMCHAGUA TENA DK.DAU 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (ISSA) chini ya Umoja wa Mataifa Bw. Hans- Horst Konkolewsky  akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani K. Dau  kwa kuchaguliwa tena kuendelea na uongozi katika Shirikisho hilo.  Dk. Dau alichaguliwa tena kuwa mwakilishi wa Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kipindi cha miaka mingine mitatu (2013-2016) huko Doha, Qatar katika mkutano mkuu wa ISSA. (Na Mpiga Picha Wetu)

Article 0

$
0
0
VIINGILIO MECHI YA TANZANITE NA AFRIKA KUSINI VYATAJWA
MASHABIKI watakaoshuhudia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini watalipa kiingilio cha sh. 1,000. 

 Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Kiingilio cha sh. 1,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange. Viingilio vingine kwa mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000. 

 Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani. Boniface Wambura Mgoyo Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Article 1

$
0
0
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC DKT. STAGOMENA TAX IKULU DAR ES SALAAM LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa DADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo leo, Dec 2, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa DADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo leo, Dec 2, 2013. Kushoto ni Ofisa Mawasiliano, Charles Mubita.

Article 0

$
0
0
KOCHA WA SIMBA AANZA KIBARUA
 Kocha Simba, Zdravko Logarusic akiwasili kwenye mazoezi ya timu hiyo  katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam. Kocha huyo amesaini mkataba wa miezi sita kuchukua nafasi ya Abdallah Kibadeni.
  Zdravko Logarusic akiingia uwanjani kuanza kazi yake.
Akiwasalimia mashabiki wa Simba.
 Akisalimiana na viongozi wa Simba.
 Wachezaji wa Simba wakijitambulisha kwa kocha wa timu hiyo kabla ya kuanza mazoezi.
 Zoezi la kujitambulisha kwa kocha likiendelea.
 Wachezaji wa Simba wakimsikiliza kocha mpya wa hiyo, Zdravko Logarusic wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
 Maelekezo ya kocha.
 Kusikiliza maelekezo.
 Wachezaji wakianza mazoezi.
 Aliyekuwa kipa wa timu ya Yanga, Yew Berko (kushoto) akijifua na wenzake wakati ea mazoezi ya Simba.
 Aliyekuwa kipa wa timu ya Yanga, Yew Berko (kushoto) akijifua na wenzake wakati ea mazoezi ya Simba.

Article 7

$
0
0
Wasanii watamba Uhuru Marathon
Katibu wa Kamati ya maandalizi ya Uhuru Marathon Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi na wasanii watakaoshiriki kwenye mkesha wa Uhuru utakaofanyika viwanja vya Leaders Club baada ya kukamilika kwa mbio za uhuru. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui akifafanua jambo.

Na Mwandishi Wetu

ZIKIWA zimebaki siku chache kwa ajili ya shindano la mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, kufanyika, wasanii watakaotoa burudani siku ya mkesha wa uhuru wameapa kufanya kweli.
Wasanii wanaotarajiwa kutoa burudani ni Roma Mkatoliki, Joh Makini, G Nako, Nick wa Pili, Mrisho Mpoto, TMK Wanaume, Mfalme Siboka na kundi la Twanga Pepeta.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema wanashukuru kupewa heshima kubwa kutumbuiza siku hiyo na hasa ukichukulia umuhimu wa amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.

“Nitafanya makamuzi ya kweli siku hiyo na watu wategemee mistari iliyokwenda shule,” alisema Roma Mkatoliki, huku Mrisho Mpoto akidai ana vitu vikali zaidi atakavyoweka hadharani siku hiyo.

Naye Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, homa ya mbio hizo imepanda, hasa baada ya kujitokeza kwa wanariadha wengi wa mataifa mbalimbali.

Melleck alisema, mbali na wengi kujitokeza bado anaamini wengi wataendelea kujiandikisha ili kufanikisha lengo la mbio hizo.

Alisema usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.

Article 6

$
0
0
BLUE SKY MEDIA KUSHIRIKIANA NA STATUS COMMUNICATIONS
Rais wa Blue Sky Media, Richard Signeski akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu ushirikiano walioingia na Kampuni ya Status Communication ya kuwawezesha waandaaji kuuza filamu kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. (Picha na Francis Dande)
Omary Salisbury (kulia), akizungumza na waandishi wa habari.

Na Elizabeth John

KAMPUNI ya Status Communication imetangaza kushirikiana na kampuni ya usambazaji wa filamu ya Kimarekani, Blue Sky Media ili kuwawezesha waandaaji kuuza filamu kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.


Baadhi ya mitandao ambayo itatumika kusambaza filamu hizo ni ITunes, Microsoft, You Tube, RAIN na mitandao mingine ya kimataifa.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski, alisema ushirikiano huu utawafanya watengeneza filamu kutoka Afrika Mashariki na Kati kuweza kuuza filamu moja kwa moja kwenye mitandao mikubwa ya usambazaji Dunia nzima.


“Lengo la ushirikiano huu ni kuwapa  watengeneza filamu kutoka nchi hizo kuweza kuuza filamu zao moja kwa moja kwa watazamaji Dunia nzima,” alisema.


Alisema wameamua kuja Tanzania baada ya kugundua kwamba hapa kuna watengeneza filamu wengi wanahofia kuwekeza fedha nyingi kwenye utengenezaji wa filamu zao kwani wengi wanahofia uchache wa masoko ya kuuza filamu zao.


“Watengeneza filamu za hapa nchini, nawaomba watengeneze filamu mjitokeze kwa wingi ili muweze kuuza filamu dunia nzima kwa urahisi,” alisema Signeski.


Naye Mwakilishi wa Status Communication, Monalisa Shayo, alisema ushirikiano wao na Blue Sky ni moja ya ushirikiano na kampuni ya Kimataifa wanaotaka kuingia katika soko la Afrika Mashariki na Kati.


“Mwaka huu umekuwa na neema kwetu kwani tumeweza kuingia mkataba na makampuni mbalimbali ili kuweza kuingia soko la Afrika Mashariki, fursa hii ni muhimu kwa watengeneza filamu wan chi hizi kuuza filamu kwenye masoko tofauti.
Viewing all 19278 articles
Browse latest View live




Latest Images